Zitto: CCM imechanganyikiwa

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechanganyikiwa na sasa kimepoteza mwelekeo wa kutatua matatizo makubwa yanayoikumba Tanzania hivi sasa.

Akizungumza katika Mkutano wa Kidemokrasia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Zitto alisema kuchanganyikiwa huko kwa CCM ndiko kunakosababisha serikali ya Rais John Magufuli iseme mengine na katika utekelezaji wake yafanyike mambo mengine.

“Tunatambua kuwa serikali ya Rais Magufuli imeweka mkazo katika kujenga viwanda. Hili ni jambo jema kwa kuwa likitekelezwa vizuri litachochea ukuaji wa ajira kwa vijana nchini. Hata hivyo, pamoja na nia njema, haielekei kwamba serikali ya CCM inaelewa namna ya kutelekeleza lengo hili zuri.

“Kutokana na mkanganyiko wa kifalsafa, serikali haijui ni nani hasa anapaswa kujenga viwanda kati ya serikali yenyewe na sekta binafsi. Matokeo yake imekuwa ikivizia miradi ya sekta binafsi na kukimbilia kuizindua wakati huo huo serikali ikitoa kauli ambazo zinarudisha nyuma ari ya wafanyabiashara wazalendo kuwekeza katika viwanda,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Mkutano wa kidemokrasia ni kikao pekee rasmi cha kikatiba katika chama cha ACT- Wazalendo ambapo viongozi na wanachama wanakutana ana kwa ana na kubadilisha mawazo kuhusu chama na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Mkutano huo wa kwanza na wa aina yake hapa nchini umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nchi na vyama marafiki kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika nyanja mbalimbali.

Zitto ambaye amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 15, alisema nchi sasa inahitaji mwelekeo, falsafa na namna mpya ya kutatua matatizo ya Tanzania; akisema CCM kwa sasa haina mwelekeo wowote – miaka takribani 25 baada ya kuachana na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho, Posta, jijini Dar es Salaam, Zitto alitoa mifano ya masuala mbalimbali yahusuyo uchumi, ajira, jinsia na elimu kupitia hotuba yake iliyokuwa na maneno takribani 5000.

Kuhusu vita dhidi ya rushwa inayoendeshwa na serikali ya Rais Magufuli, Zitto alisema ACT kinaunga mkono juhudi hizo ingawa hadi sasa wanaoshughulikiwa ni mawakala wa rushwa walioko serikalini na si wala rushwa wenyewe.

Mwanasiasa huyo pia aliponda mwenendo wa serikali wa kuzuia shughuli mbalimbali za kisiasa na kusema hakuna namna ambayo nchi inaweza kupambana na ufisadi pasipo kujali misingi mingine ya haki za watu.

“Mtu yeyote anayedai kwamba anaweza kupambana na ufisadi na kuleta maedeleo kwa kukanyanga demokrasia na utawala wa sheria ni mwongo na anastahili kukataliwa na kukemewa mapema kabla hajaota pembe.

“Tunasisitiza kuwa mtu yeyote wa kawaida au kiongozi anayesema kwamba anaweza akapambana na ufisadi kwa kukanyaga misingi ya demokrasia na utawala wa sheria mtu huyo ni fisadi na anataka kujenga himaya mpya ya ufisadi. Mtu huyo, pamoja na mambo yake yote, yafaa akataliwe na kudharauliwa haraka,” alisema.

Katika hatua nyingine, Zitto alisema kwamba juhudi za kuboresha elimu hapa nchini zitakuwa na maana tu endapo walimu ndiyo watakuwa kipaumbele na si madawati wala madarasa. Alisema upatikanaji wa madawati na maabara utakuwa na maana tu endapo walimu watakuwa na motisha ya kufanya kazi.


“Tafiti zinaonyesha kwamba ili kuboresha ubora wa elimu kitu kikubwa na cha msingi kabisa kuliko vyote ni kuwekeza kwa walimu na taaluma ya ualimu. Maeneo muhimu ni mafunzo ya walimu na kuhakikisha kwamba wanakuwa na motisha wa kutosha katika kufanya kazi zao. Bahati mbaya hapa Tanzania serikali na jamii kwa ujumla hatuthamini kazi ya ualimu.

“Taaluma ya ualimu imekuwa ni daraja la kujiokoa baada ya kukosa sehemu zingine. Walimu wetu wanaofundisha katika mazingira magumu sana hatuwathamini na wakati mwingine hata tunawabeza.

Pia alitoa wito kwa asasi za kijinsia kupigia kelele suala la ajira kwa wanawake kwa vile alisema hivi sasa wanaume wanapata ajira zaidi kuliko wanawake, jambo alilosema linapaswa kurekebishwa.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alitumia fursa hiyo kueleza kuhusu changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini; akisema zaidi ya theluthi mbili ya nguvukazi iiyopo nchini haijaajiriwa katika sekta rasmi.
Mbele ya waliohudhuria mkutano huo kutoka ndani na nje ya nchi, Zitto alieleza kusikitishwa kwake na mwenendo wa nchi za Kiafrika katika siku za karibuni, aliosema unafanana na hali ilivyokuwa kwenye miaka ya 1960.

“Tunashuhudia uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu katika mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani ya Kusini na Ethiopia. Machafuko yote haya yanasababishwa na kupuuzwa kwa haki za kiraia na kidemokrasia.


“Tunatoa wito maalumu kwa taasisi za kiraia, taasisi za dini na vyuo vikuu katika bara la Afrika kusimama imara katika kulinda utawala wa sheria na demokrasia ya vyama vingi. Tunazitaja taasisi hizi kwa sababu kazi zao na uwepo wao unategemea sana uwepo wa demokrasia katika nchi yoyote duniani. Demokrasia ya vingi ikichezewa na hatimaye kufififshwa taasisi za kiraia, taasisi za dini na vyuo vikuu haviwezi pia kuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa uhuru.

“Chama chetu kinamtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila aheshimu Katiba ya nchi hiyo na kuruhusu uchaguzi kufanyika kama ilivyopangwa ili kuwezesha mpito wa kidemokrasia kwa amani kabisa. Tanzania haiwezi kuendelea kupokea wakimbizi wa kongo kwa makosa ya wanasiasa wanaong’ang’ania madaraka kinyume na Katiba,” alisema Zitto.

Mwisho

Chanzo: Ukurasa wa FB wa ZZK

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ovyoooo.hana jipyaa..angalia siasauchwara za kiafika..anampona magufuli badala ya kumsuport na kumuunga mkono..anavyojikanyaga mwenyewe ovyoooo..na bado magufuli fanya kazi yako na Mungu akubariki...

    ReplyDelete
  2. Zitto, Mie Ajira yako ninayo!! Na pakukuweka ninapo (Yaani pa wewe kuishi kumalizia Maisha yako) Guess Where? Mirembe!!!!! Karibu sana Tunakusubiri .. Huko Fwezi Buku.. Unijulishe lini unatarajia kufika ili tuweze kukupokea bila kuchelewa na Kumtaarifu Warden hapa Mirembe Isanga. Hapa Kazi Tu

    ReplyDelete
  3. Mie hata Sielewagi.

    Zitto CCM imechanganyikiwa
    CCM Zitto Kachanganyikiwa
    Kachanganyikiwa Zitto Kwa CCM

    Zote naona ni ile ile.. Dogo embu fafanua. Siasa uchwara huziwezi. Tumzika nangoja ufafanuzi.

    ReplyDelete
  4. Hii Picha naikumbukaga... Ulikuwa Dalasa la Ngapi vile?

    ReplyDelete
  5. Hii Picha naikumbukaga... Ulikuwa Dalasa la Ngapi vile?

    ReplyDelete
  6. Kuna Tetesi tumesaikia Unatafuta Kadi za Uanachama Wa CCM huko TABATA, Je ni Kweli?
    Usiwawache wenzako kwenye MATAA ukaingia MITINI KAbwe.
    Huo si UUNGWANA. Kama ni kweli hata kama imekula kwako Zitto. Unamezea.. Huko CCM serikali yake in spidi siyo ya kawaida.. Wewe utakuwa Majeruhi .. Bora Ushangilie TU.
    Hapa Kazi Tu na Baba JPJM.

    ReplyDelete
  7. Heheee. Zito Kabwe give us a blek time na hizo siasa zango za bongo fravour. Kila siku wewe ccm hivi ccm vile. Leta sasa wazo la nini? Kifanyike cha maendeleo ya nchi yetu Tanzania ili ipate kusonga mbelee kitaifa mpka kimataifa tumechoka kuchekwa na kuambiwa nchi za dunia ya tatu. IQ INTELLIGENT QUILT ni ndogo

    ReplyDelete
  8. cc wa~tz tuna kila sababu ya kukosoa panapo mabaya na kusifia mazuri, tuache ushabiki wa kivyama, ila sioni ajabu hata baba mzazi/mlezi aweza kukosea tena kwa kudhalilika KABISAA LAKN ni vigumu kukuta unamkosoa badala yake unamtetea..,, JPM kuna sehemu yuko vizuri KABISAA lakn kuna mistake KADHAA huwa anazifanya,,, lakini MJUE KUWA chake MTU hukosolewa na majirani kama una akili usiwatusi angalia wapi wanapokukosoa nawe jirekebishe tuu.... kazi ya upinzani HAPA NCHINI ni hyo ya kushauri,kukosoa,kupendekeza, na kutoa mielekeo ya hali za kiuchumi/kisiasa/kijamii/ na kidiplomasia, sasa mzazi/baba akiziba midomo ya watoto, mama mwenye nyumba, majirani, marafiki na jamaa HATA iwe ki~nguvu au kisaikolojia ni wazi kuwa anabomoa haki/uhuru WA kutoa maoni/ ushauri na misingi ya demokrasia ya familia husika, ila Niseme "HAPA KAZI TU" ,,,, Kama Ni Haki Kuongea HAYA NA KUCHANGIA MADA KAMA HIVI, Ni Wazi KUWA Sitatafutwa. NAWATAKIA MAJUKUMU MEMA WAUNGWANA NA ALLAH ATAWALINDA KWA KILA LA KHERI..... INSHAALLAH,,,...,,,

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousOctober 9, 2016 at 6:57 AM nakuunga mkono, kila mtu ana haki ya kutoa maoni, sidhani kama ni sawa kumtukana Zitto, na kwa wale wanaomtukana sijaona hoja nzito wanazotoa hadi Zitto aonekane wa ajabu, jaribuni kutoa hoja za maana sio maneno ya ajabu kama hayo.

      Delete
    2. Tatizo watanzania tumekalia ushabiki sana,sasa kuna kibaya zito kaongea?

      Delete
    3. HUNGRY-FACE, Zitto , Nakuonea Huluma , ile bajaji ukipanda halafu unakatisha balabala ya mwendo kasi. HATARI mwangu..Wengine huwa miguu wako Moi. na wengine bahati mbaya hupoteza loho. Wewe ndiyo kwanza Julai umepata Jiko.. Hembu wacha na haya ya upuuzi usiyo yaweza ili ufanye kweli hapo nyumbani upate wa kucheza nae.. Itakuwa ni la maana sana kulikoni haya ya uchwara yamekushinda... Kuwa lijali ..usipo angali Mbwee atakusakama tena... matokeo hayatokuwa bila bila safari hii..Chunga Mwanangu...Je utakuwa miaka mingapi 2025 ? Labda sukari na plesha angalia afya yako na jitahidi ufanye ploduktion kunyumba..

      Delete
  9. Wewe ndio umechanganyikiwa hujui la kufanya

    ReplyDelete
  10. jamani ccm imechanganyikiwa au zito wewe bwana bora wakupeleke mirembe au uwekwe ndani cos unaleta uchochezi tunataka amani hebu tuachie tanzania yetu sijui wewe ni wa wapi bora urudi kwenu aisee tunataka amani amani wacha kuropoka ovyo

    ReplyDelete
  11. Hivi mbona hamjui namna ya kumalizana na wapuuzi muulizeni JPM atawapeni,,, NI KUWAPUUZA NA KUTOWAJIBU KWA KILA WANACHOSEMA na dawa hii ina maumivu makali angalieni!!! Ni bora upigwe za uso kuliko kupuuzwa inauma sana
    Mpuuzeni huyu hungry-face na atakwisha tu,,,kila siku anakuja na ndoto zake bora angesoma fizikia angepata kazi ya ualimu!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Umenikosha Huyu HUNGRY -FACE -- NI CRY BABY LAZIMA TUMTAFUTIE PIPI LOLIPOPU. ITAMSHUGHULISHA KU MUMUSA. ATAKUWA KIMYA..ANABOA SANA LA MAANA HANA..

      Delete
  12. mhh wewe zito kwa kweli huna kazi wala siasa haikufai mwenzangu naona unajichanganya mwenywe hivo we kweli ni mwana siasa? shule gani ulienda bwana unatutia aibu bora funga kibwebwe uingie jikoni tunataka amani

    ReplyDelete
  13. huyo bwana anakera haswa yaani hata ukimuangalia ule uso wake unakirihika kabisa yaani hata hanaga aibu jitu zima zozota huna lingine mpuuzi wewe usituharibie nchi yetu tanzania imetulia na sifa zake oeke yake amani kabisa hivo wewe utakuwa lini tuaichie nchi yetu ushaambiwa rudi kwenu

    ReplyDelete
  14. Kipi bora ccm au JPM!! Atujawahi kupata rais kama JPM Afrika nzima. Mungu mlinde na muongoze JPM.

    ReplyDelete
  15. Tena Zito , Nakuonea Huluma , ile bajaji ukipanda halafu unakatisha balabala ya mwendo kasi. HATARI mwangu..Wengine huwa miguu wako Moi. na wengine bahati mbaya hupoteza loho. Wewe ndiyo kwanza Julai umepata Jiko.. Hembu wacha na haya ya upuuzi usiyo yaweza ili ufanye kweli hapo nyumbani upate wa kucheza nae.. Itakuwa ni la maana sana kulikoni haya ya uchwara yamekushinda... Kuwa lijali ..usipo angali Mbwee atakusakama tena... matokeo hayatokuwa bila bila safari hii..Chunga Mwanangu...Je utakuwa miaka mingapi 2025 ? Labda sukari na plesha angalia afya yako na jitahidi ufanye ploduktion kunyumba..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad