Aunt Ezekiel: Achana na Mimi Wewe Wema Sepetu

MASTAA wawili waliokuwa mashosti siku za nyuma, Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wameingia kwenye msuguano tena hivi karibuni huku hali ikionesha kuwa mastaa hao kwa sasa ndiyo basi tena.

Hali hiyo imetokea juzi baada ya Aunty kuweka picha ya kumtakia siku njema ya kuzaliwa rafiki na msanii mwenzake, Maimartha Jesse kwa kuandika, “Happy bday Kipenzi cha Roho yangu …..Unajua kama Nakupenda cha zaidi Naomba Yesu Akutunze milele.”

Katika post hiyo, followers kadhaa wa Aunty walikomenti akiwemo staa mwenzake kwenye tasnia hiyo, Wema Sepetu aliyekomenti “Yesu atamtunza…” Baada ya hapo, Aunty akaibuka na kumtolea povu Wema akimchana “Achana na mm ww @wemasepetu“ hali iliyoibua maswali na mijadala mingi mitandaoni, huku watu wakitaka kujua kwa nini Aunty amemshushua hivyo Wema.

Inasemekana kwamba, chanzo ni Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Wema kumsema vibaya Aunty kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Kwa hali ilivyofikia mpaka sasa inaonesha sio rahisi tena kwa waigizaji hao kuelewana.

Tangu siku za hivi karibuni, Wema alipokosana na rafiki yake Muna Love na kumsema vibaya kwa kutumia video aliyojirekodi na kuisambaza mitandaoni, Wema kwa sasa amekuwa akijitahidi kuwa karibu na Aunty ili warudishe urafiki wao wa zamani japokuwa jitihada zake zinaonesha kugonga mwamba baada kuambulia maneno mazito kutoka kwa Mama Cookie.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani tangu Aunt Ezekiel ajifungue Wema hata hajawahi kwenda kumuona mtoto Wake halafu sasa hivi kakosana na Muna ndiyo anajikomba kwa mama Cookie, inaonekana Wema anajijali mwenyewe tu akiwa na matatizo ndiyo anawakumbuka rafiki zake wa zamani, Wema ukae ukijua sio kila kitu ni kuhusu wewe tu,huyo rafiki yako wa zamani mama Cookie pia yeye ni binadamu kama wewe wakati anajifungua ukakaa kimya hata kwenda kumjulia hali hukutaka halafu leo hii unajikomba kwake, mama Cookie umempatia jibu zuri sana kuwa aachane na wewe

    ReplyDelete
  2. Annon hapo juu sawa kabisa, yes it's not about her. Snura, Kajala, Aunty na Muna msiwe maboi wa Wema. Salute Aunty kwa kujielewa.

    ReplyDelete
  3. URAFIKI NI PESA.MAMBO YAKIWA POA WOTE MARAFIKI WAKUAZIMANA NGUO NA MAPAMBO.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad