Bibi Mbaroni Kwa Kumlisha Kinyesi Mjukuu Wake

MWANZA: BIBI mmoja aliyejulikana kwa jina la Amina Hamisi (56) mkazi wa Mtaa wa Mahina, Kata ya Butimba, Jijini Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kumlazimisha mjukuu wake Rehema Sadiki (7) kula kinyesi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Augustino Senga amedai kuwa tukio hilo limetokea Novemba 11, mwaka huu ambapo mtoto huyo alikwenda chooni kujisaidia na kushindwa kumwagia maji ili kuondoa kinyesi chake ndipo bibi yake ili kumuadhibu alimuamuru kula kinyesi hicho kitendo ambacho mtoto huyo alikitekeleza.

Baada ya tukio hilo kutokea raia wema walitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.

Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa jiii la Mwanza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo vya kikatili hasa kwa watoto wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni kosa kisheria hivyo wananchi waache kufanya vitendo hivyo na watakao bainika sheria itachukua mkondo wake.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Shetani huyu bibi,angekutana na mimi angepata bakora za nguvu kiisha ningemlisha na yeye kinyesi bila kujali umri wake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad