Tokeo la picha la thomas mashali
Ally alisimulia mkasa wa rafiki yake huyo akiwa msibani maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam, ambapo amedai kuwa juzi usiku alipata taarifa za kushambuliwa kwa Mashali na watu wasifahamika maeneo ya Kimara jijini humo.
“Ilikuwa usiku nimekaa nyumbani Manzese Madizini akaja dereva bodaboda anaitwa Yusuf Kidevu akaniambia babaako wanampiga huko Kimara wanamuua kama vipi nenda.”
“Nikahisi ni uongo kwasababu wakati mwingine wanazusha tu, mara kidogo akaja mtu wa pili akasema babaako anakufa huko Kimara, kwasababu alikuwa ni mtu wa pili kuniambia nikaona bora niende.”
“Nikaenda hadi Kimara, kufika pale nikakuta wameshampiga wamemuumiza askari wanampakia kwenye gari. Nikalifata gari hadi Sinza, akapata kitanda akalazwa nikaenda kumsalimia lakini saui ilikuwa inatoka kwa mbali hadi usogeze sikio ndio unaweza kumsikia.”
“Nikamuuliza imekuwaje, akasema kuna dereva bodaboda alimkodi lakini walivyofika Kimara akampa hela kidogo wakaanza kuzozana ndio mkasa ulipoanzia.”
“Alimpa shilingi 2000 lakini dereva bodaboda alikuwa anataka shilingi 3000, akaanza kumtukana Mashali akaona anadharauliwa akampiga ngumi yule dereba bodaboda akaanguka chini, baada ya hapo akaanza kupiga kelele za mwizi wakaja watu wengine watatu wakataka kumpiga akapambana nao akawapiga.”
“Baada ya kuona wote hawamuwezi wote wakaanza kupiga kelele za kumuita mwizi, wakaongezeka watu wengine wakaanza kumshambulia.”
Mwili wa Thomas Mashali unatarajiwa kuzikwa Jumatano jijini Dar es salaam.
" Alimpa 2000 na dereve alitaka 3000" Kumbe alikuwa ni mwizi. Msitake kutetea maovu.
ReplyDeleteAcha ujinga wewe sasa ndio umeona sababu ya kutoa uhai wa mtu.Vyombo vya sheria vipo mob justice haifai.
DeleteAnoni wa kwanza inaelekea unaweza ua kwa 200 pole sana asee!!!!!
DeleteNae huyo mashali ndo alitumia huo ubondia wake mana niashara ni kupatana tu sio kwavile ni bondia ujione naweza fanya lolote bila mtu kuniweza. Angepatana nae tu kabla hajapanda hio bajaji sijui bodaboda lakini nae huyo mashali alijua lolote mimi ni bondia akinifanyia nisilotaka nitampiga yeye dereva hana kosa kadai haki yake na ni uongo hakupatana nae mana angepatana nae tokea safari haijaanza kusingetokea mapigano yaliopelekea mauwaji hayo. Ubondia jamani ni ulingoni sio mitaani na ktk biashara za watu.
ReplyDeleteVyombo vya sheria vipo wapi?? Rushwa, uonevu nk
ReplyDeletekweli ni heri wangepatana kabla hajapanda sababu bongo ya leo kitu kidogo tu unaitiwa kuwa ni mwizi na kwa watu ambao mnaishi bongo hayo mtakuwa mnayafahamu sababu yanatokea kila kukicha hivyo ili kuepukana na hayo matatizo ni heri kuwa mwangalifu na makini na mkweli kama bondia angemwambia dereva boda boda kuwa mimi nina 2000 tu kabla hajapanda hapo dereva angeweza kuamua apande au asipande kuliko kunyamaza kimya hayo yote yasingetokea naona dereva boda boda kaona amepewa zarau kwenye kazi yake sababu hizo kazi hamna mtu anayependelea kufanya kazi ambayo ni hatari lakini pamoja na yote siyo mpaka wamtoe mtu uhai Wake au kuwatoa watu uhai sababu ya pesa, jamani serikali iko wapi na inafanya nini, kwa nini serikali inaangalia tu mambo haya yakitokea kila siku bila kufanya lolote kweli ni aibu kwa taifa maana mambo haya ya mauaji bongo yanazungumziwa sana Ulaya na Marekani mpaka watalii wanaogopa kuja bongo kuona vitu hivi vikitokea
ReplyDeleterip bROTHER HAYA MAMBO YANASIKITISHA SANA
ReplyDeleteSo sad!
ReplyDelete