Sinema ya model Calisah imezidi kushika kasi – amefunguka kwa kudai kuwa ni yeye au Wema Sepetu ndio waliovujisha video inaowaonesha wakilana denda.
Siku chache zilizopita mwanamitindo huyo wa kiume alikamatwa na polisi kwa kosa la kudaiwa kusambaza kipande hicho cha video lakini baadae aliachiwa.
Akiongea na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, Calisah amesema, “Nilienda kwa Wema tukawa tunaongea vizuri tu najaribu kumuelezea, lakini hata yeye alishangaa kuona polisi wameingia. Si yeye ni wapambe wake ndio walienda kituoni, wabeba pochi tu, tena afadhali wangekuwa wanawake ni wanaume.”
“Picha zile tunazo mimi na yeye, kwa hiyo kama sio mimi niliyesambaza ni yeye na kama sio yeye ni mimi. Mimi sijasambaza siwezi kumdhalilisha mwanamke kiasi kile. Sasa hivi nampenda kama mshikaji kwa sababu tayari nina mwanamke mwingine ninayempenda,” ameongeza.
Umemtumia tunajua. Na sasa ni mshikaji tu sio? Thirst for fame! Shame on you.
ReplyDeleteumemtumia mtoto wa watu, shame shame on you
ReplyDeleteJamvi la wageni hilo hakuna cha kumtumia mtoto wa watu wala nini hapo
ReplyDeleteWaswahili wa kale walisemaga ngoma ikivuma sana hupasuka wala hata hawakukosea kabisa
ReplyDeletemdomo nje nje kudendeka, wa kumlaumu nani? ukisha amua kuwa na mahusiano na kila anayepiga hodi basi mwili wako umeufanya public, na picha mtandaoni ni sehemu ya public, tunachoshangaa na kulalamika ni kipi hapo?
ReplyDelete