Calisah Afunguka Kuhusu Mtu Aliyevujisha Video Akilana Mate na Wema Sepetu

Sinema ya model Calisah imezidi kushika kasi – amefunguka kwa kudai kuwa ni yeye au Wema Sepetu ndio waliovujisha video inaowaonesha wakilana denda.

Siku chache zilizopita mwanamitindo huyo wa kiume alikamatwa na polisi kwa kosa la kudaiwa kusambaza kipande hicho cha video lakini baadae aliachiwa.

Akiongea na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, Calisah amesema, “Nilienda kwa Wema tukawa tunaongea vizuri tu najaribu kumuelezea, lakini hata yeye alishangaa kuona polisi wameingia. Si yeye ni wapambe wake ndio walienda kituoni, wabeba pochi tu, tena afadhali wangekuwa wanawake ni wanaume.”

“Picha zile tunazo mimi na yeye, kwa hiyo kama sio mimi niliyesambaza ni yeye na kama sio yeye ni mimi. Mimi sijasambaza siwezi kumdhalilisha mwanamke kiasi kile. Sasa hivi nampenda kama mshikaji kwa sababu tayari nina mwanamke mwingine ninayempenda,” ameongeza.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umemtumia tunajua. Na sasa ni mshikaji tu sio? Thirst for fame! Shame on you.

    ReplyDelete
  2. umemtumia mtoto wa watu, shame shame on you

    ReplyDelete
  3. Jamvi la wageni hilo hakuna cha kumtumia mtoto wa watu wala nini hapo

    ReplyDelete
  4. Waswahili wa kale walisemaga ngoma ikivuma sana hupasuka wala hata hawakukosea kabisa

    ReplyDelete
  5. mdomo nje nje kudendeka, wa kumlaumu nani? ukisha amua kuwa na mahusiano na kila anayepiga hodi basi mwili wako umeufanya public, na picha mtandaoni ni sehemu ya public, tunachoshangaa na kulalamika ni kipi hapo?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad