Dadapoa 25 Mbaroni Kwa Kujiuza Moshi

Watu 66 wakiwamo wanawake 25 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya kuuza miili maarufu kama dadapoa katika maeneo mbalimbali ya mjini Moshi, wanashikiliwa na polisi.

Licha ya kuwashikilia wanawake hao, polisi wamewakamata wafanyabiashara saba wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya na watumiaji.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita amesema watu hao walikamatwa Novemba 26 saa mbili usiku kwenye maeneo ya katikati ya mji katika operesheni ya kutokomeza biashara hizo haramu.

“Tukiwa na Diwani wa Mawenzi, Hawa Mushi tulishirikiana kuwakamata wahalifu mbalimbali katika mji wetu maana nyakati za usiku kuna mambo yanafanyika ambayo tusipoweza kuyakabili  mapema yanaweza kuleta madhara baadaye,” amesema Moita.

 Moita amesema baadhi ya wafanyabiashara wadogo ndiyo chanzo cha kuuza dawa za kulevya na huwaficha wanawake wanaofanya biashara ya miili yao usiku.

“Tumewakamata wanawake wanauza miili yao 25, wafanyabiashara wanaowalinda wanawake hao na kuuza dawa za kulevya saba na walikutwa wakitumia dawa hizo nao wako saba,” amesema Moita.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad