Diamond Atoa Jibu la Utata Kufuatia interview ya Ommy Dimpoz

Inaitwa Tit for Tat! Baada ya Ommy Dimpoz kueleza kwa kina kuhusiana na sababu iliyopelekea wakakosana na Diamond, muimbaji huyo wa Salome, amejibu kupitia Instagram.

Majibu ya Diamond ni ya mafumbo kiasi na tayari yamepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki huku wengi wakichukizwa na kauli yake.

Ameandika:

Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi…. Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???😟 hii nayo ni #KOKORO ujue

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu Domo kashajisahau na kujiona yeye ndo Malika na kutukana wenzie wasenge.Dunia ni mapito tuliwaona wengi kabla yako.

    ReplyDelete
  2. Tema mate chini mungu hajawahi kukosea na hata siku moja hatakuja kukosea kumbuka

    ReplyDelete
  3. huo sio ungwana duu kumbe Naseeb uko hivo hawezekani mtu kwenye interview aonge uongo wewe una roho mbaya sana Mungu anakuona sasa anakuwezesha anakupima huo ni mtihani sasa subiria majibu rudi kwa mola wako wacha chuki kumbuka ulikotoka

    ReplyDelete
  4. Acheni kelele si hua watu wanampelemba wenyewe mlitakaje asiseme akae kimya mumuone zuzu.....na hata angekaa kimya mngesema ana kuburi kwa sababu ya mafanikio aliyo nayo. Hamumsemi Dimpoz aloanza maneno ya shombo mnakomaa na aliyejibu mapigo nyie mmerogwa nini.......ipo siku ipo siku, kalewa sifa kalewa sifa.....roho za kwa nini zimewajaa tu hamna lolote. Mlifurahishwa na ujinga wa dimpoz mlidhani hawezi kutoa ya shombo naye.....alaaaaaaaaaahhhhh

    ReplyDelete
  5. Aiseee unasema Mungu kakosea wewe kijana wewe kakosea mahesabu eti eeeh haya..hebu kimbia msikitin katubu b4 hasira yake haijashuka....yan kimbia we unajua Allah anatoa neema kwa njia gani hebu uwe unanyamaza....

    ReplyDelete
  6. hamna shombo wala hakuna alie rogwa wacha ujinga kawaida ukweli unauma ila binadamu huwa tunajisahau tulipotoka mbona naseeb kasahau mengi tu wliompa umaarafu wote kawasahau haya alie juu tunamsubiri. Omy kanena ukweli ndio maana naseeb hana la kusema ila kujitetea kwa ujanja just kumbuka ulikotoka na waliokutoa na uliokuwa nao na kukujali wakati uko chini ukisha jitambua then utapata jibu

    ReplyDelete
  7. naseen ukubali ukweli una roho mbaya selfish wewe kama ulikuwa ni mtu ungewashkuru wanaweke waliokusaidia katika maisha yako waliokutoa na wakakustarabisha na hilo umelisahau tumeshakujua una roho mbaya hata usime ni i ukweli ukidhihiri uwongo unajitenga ugopa Mwenyezi Mungu

    ReplyDelete
  8. kwanza ulijulikana wakati uko na Wema akakupa kiki then ukarukia kwa kidoti then peny wote shoga zake wema alafu ukarudi tena kwa wema akakumilishia umepata umaarufu kwa mgongo wa Wema Sepetu hivo unalipi la kusema hata english umejifundisha wakati uko na wena then penny akakuwekea mwalimu ikiwa umesahau hisani hii ndio ilio kufanya ufuke ulipofika kweli wewe ni mtu wa aina gani? au kusema uongo na kudanganya wenzako kwa kuwa ulijua ukimtoa omy atatoka na atakushinda ikabidi umtolee nje usisahau hapo ulipo ni kutokana na migongo ta wenzio inabidi uwashkuru sio kuleta kokoro zako

    ReplyDelete
  9. Dah! Hebu muachage ujinga wa kumshirikisha Mungu kwenye mambo yenu ya kijinga. We Dai hebu jifunze kuangalia unachoongea, sasa kwahiyo unampangia Mungu wa kumpa na wa kumnyima? Kwahiyo we unajiona amekupa kwa vile unastahili sana kupata kuliko wengine? Be humble maaaaaaaan maana kuna waliostahili kupata zaidi yako ila hawajapata. Ni Mungu tu aiseee

    ReplyDelete
  10. tatizo elimu, hata mtu uwe umefanikiwa vipi, elimu yako ikiwa ndogo unashindwa kujitambua, jamaa kaishia darasa la saba, sasa kaona yeye katoka kwahiyo kuwadharau waliomsaidia ndo jibu lake!!

    ReplyDelete
  11. duuh interview imeniamsha siamini kumbe Diamondi uko hivi wewe kweli mtoto wa tandale

    ReplyDelete
  12. mungu hajawhi kukosea hesabu zake hata siku moja na wala haitatokea milele na milele ww kufanikiwa sio kwamba mungu kakupendelea elewa kuwa mungu hana upendeleo sisi sote kwake ni sawa ndo maana sote tunakufa na tukifa tunazikwa chini hakuna tajiri wala mtu yoyote aliyemaarufu duniani alizikwa angani mungu si wa mchezo mchezo utakuja lia km mbwa kichwa chini miguu juu ila sijui kwanini wadamu tukipata huwa tunawadharau wasiokuwa nacho

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad