Edward Lowassa Afafanua Kutoonekana Kwake Misiba ya Sitta na Mungai

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu kutoonekana kwake kwenye misiba ya viongozi wawili wa zamani serikalini, Samuel Sitta na Joseph Mungai.

Sitta, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, alifariki dunia Novemba 7, akiwa Ujerumani alikokwenda kutibiwa tezi dume na siku iliyofuata alifariki Mungai, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Gumzo kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa ni kutoonekana kwa Lowassa, ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Lowassa aliliambia gazeti hili jana kuwa, kilichomkwamisha kufika kwenye misiba hiyo ni kuwa safarini Afrika Kusini alikokwenda kumuangalia mdogo wake, Bahati Lowassa aliyekuwa mgonjwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad