Tarehe 9, Novemba 2016 siku moja baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Marekani, aliyekuwa mgombea wa Chama cha Republican Donald John Trump alitangazwa kuwa mshindi baada ya kumgaragaza mpinzani wake wa karibu na mgombea wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton.
Baada ya kutangazwa kuwa Rais Mteule wa Marekani, vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo vinawajibu wa kuhakikisha yeye (Donald Trump) na familia yake wanakuwa salama wakati wote.
Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Meya wa New York, Marekani gharama za kumlinda Trump na familia yake kwa siku moja ni zaidi ya dola milioni 1 (TZS bilioni 2.2).
Mke wa Donald Trump, Melania Trump pamoja na mtoto wao wa miaka 10, wao muda mwingi huwa nyumbani sababu ya shule kufungwa hivyo hutakiwa kulindwa muda wote huku Trump akiendelea na shughuli nyingine za serikali.
Mbali na hao bado kuna watoto wengine wa Trump na wajukuu zake ambapo wote hao wanatakiwa kulindwa na maafisa wa usalama wa Marekani.
Afisa wa Polisi katika Jimbo la New York aliwaeleza waandishi wa habari siku ya Ijumaa kuwa ulinzi wa Rais Mteule na familia yake ni suala namba moja wanalotakiwa kulishughulikia. Kazi kubwa polisi wanayotakiwa kufanya ni kutoa usaidizi kwa Maafisa Usalama wa Taifa ambao hasa ndio wana jukumu la kumlinda Rais Mteule
GHARAMA za Kumlinda Rais Mteule wa Marekeni Donald Trump Kwa Siku Moja Hizi Hapa
0
November 22, 2016
Tags