Godbless Lema na Siasa Ngumu Zisizo Wapendeza Watawala...

Kuna Godbless Lema mmoja tu hapa Tanzania kwa Africa Mashariki unaweza kumfananisha na Kizza Besigye ambaye police hawakatiki nyumbani kwake.

Hawa ni wanasiasa ambao wameamua kufanya siasa ngumu zisizo wapendeza watawala.
Ni watu ambao kusikia kukamatwa na police kwao siyo story tena Bali inaweza kuwa story siku watakapo amua kukaa kimya, Ila kusikia wapo Central police, Wanapandishwa kizimbani,Wapo Magereza hilo siyo jambo geni wala halitakuwa geni Bali tutastuka na kushangaa pindi watakapo kaa kimya tutakuwa na maswali mengi ya kujiuliza.

Ujasiri wao wa kufanya siasa ngumu za level hiyo unawabakisha kuwa Wanasiasa bora wa upinzani wakati wote wenye ushawishi Mkubwa wakati wote.

Ushawishi wao hupelekea Mara kwa Mara kwa wafuasi wao kupata shida Mara nyingi kila waenda mahakamani hukutana na vigingi vingi vingi Mara kukamatwa Mara kufukuzwa ili mradi wasionekane wapo wengi mahakamani kwenda kuwatia moyo.

Wataendelea kubaki kuwa Wanasiasa wa saisa ngumu za kiafrika ambao wameamua kupambana na changamoto hizo wazi wazi bila kuwa na chembe ya uoga....

By Henry Kilewo
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata wewe mwandishi wa habari hii ya kumsifia mtu kama Lema unahitaji kuchunguzwa akili kama huyo unayemsifia.
    Kizza hafanyi siasa za kumtukana mtu wala kumuuombea raisi wake afe kama Lema
    Chadema yote inapoteza credibility na ndio maana hata hao "Wenye Chama" hawako saana na Lema kwani ayafanyayo wao hawamo, siasa gani hizo unazozita ngumu za kutukana viongozi na kumuombea ati rais AFE ndio siasa hiyo???
    Pole sana ndugu

    ReplyDelete
  2. Siasa Ngumu gani zisizokuwa na itikadi. Siasa ni Itikadi na sio matusi. Kama ni matusi na matusi yenyewe yanawalenga watawala basi kila mtu atapaswa kuitwa mwanasiasa nguli kwa sababu ni nani asiyeyaweza matusi????? Tunachokitaka kukiona kutoka kwa hao wanasiasa uchwara ni hoja za nguvu na sio nguvu za hoja. Haingiii akilini kuona mbunge mzima ambaye wananchi wa jimbo lake wanamtegemea katika kusimamia maendeleo yao anatokea kuwa kioja kwa kumtolea lugha ya kashfa na matusi mkuu wa nchi. Huyo ndio mwakilishi gani wa wananchi.

    ReplyDelete
  3. Henery Kilewo..mimi jinsi nnavyo kujua siamini haya kama ni maneno yako. Nasema kwa utendaji wa awamu yetu hi ya tano..Huyu mtafuta kiki wa mitandao kwa uchwara wake..ukitaka hali halisi ni nilikwambia uende kule Act..manake anamjua vizuri na ufipishe huu uandishi wa masimulizi chochezi kati mtandao..heneli wacha huu upuuzi na ukome kutuletea tena..ntakuona kesho jioni..kumbuka Hakuna malipo bila kazi.. na nguvu kazi ndiyo itakayo kufanya uishi..Dili zimefungiwa kwa muda mrefu. na siasa uchwara ni wakati wa kampeni kule..2025 kama mtakua hai ubengeni HAI. I SAY HAI NA GOOD BYE..HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  4. Henery Kilewo..mimi jinsi nnavyo kujua siamini haya kama ni maneno yako. Nasema kwa utendaji wa awamu yetu hi ya tano..Huyu mtafuta kiki wa mitandao kwa uchwara wake..ukitaka hali halisi ni nilikwambia uende kule Act..manake anamjua vizuri na ufipishe huu uandishi wa masimulizi chochezi kati mtandao..heneli wacha huu upuuzi na ukome kutuletea tena..ntakuona kesho jioni..kumbuka Hakuna malipo bila kazi.. na nguvu kazi ndiyo itakayo kufanya uishi..Dili zimefungiwa kwa muda mrefu. na siasa uchwara ni wakati wa kampeni kule..2025 kama mtakua hai ubengeni HAI. I SAY HAI NA GOOD BYE..HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad