Kwako Comrade G.Lema; Najua mapito unayopitia kwasasa, ni mapito makubwa sana yenye historia kubwa inayochochea hasira na kuamsha hisia Kali.
Nataka ujue na dunia ijue upo Mahabusu siyo kwasababu ya kubaka ama kuzini, upo kwasababu umekataa uonevu,umekataa kuishi ukiwa umepiga goti umekataa kuwatukuza wasiyositahili kutukuzwa, umekataa kuwapa utukufu usiyokuwa wao wala ukuu usiyositahili kwao.
Furaha yangu nipale ninapowaona wanajaribu kutisha mtu asiyeogopa mtu ambaye wakati wote amekuwa akiyaishi Yale anayonena...
Comrade Lema... najua jambo lililopo mbele yako ni jambo dogo kwako kwa aina ya siasa zako naona wanazidi kuiambia dunia na ulimwengu aina ya kamanda wanaopambana naye...
Comrade Lema... Wewe ni shujaa wetu na itabaki kuwa hivyo, unatupa somo sisi Wanasiasa wengine namna ya kuitafuta haki bila kuipigia goti, unatupa somo kubwa sana, kama tulifikiri tumefika tusahau na tuone ndiyo kwanza tumeanza Safari ya mabadiliko, Umetuamsha ya kwamba tulikuwa tumejisahau kuna wajibu tumeupuuza kipindi Fulani...
Comrade Lema.... Jina lako lipo juu ya Mlima mrefu hakuna wakufikia kileleni pale isipokuwa Jah pekee ndiyo mwenye Mkono huwo, Maono yako ni makubwa si Rahisi Mwanadamu asiye kuwa na Imani kufikiri kuwa ni imani na imani hukaa na mwenye imani...
Comrade Lema... Mara nyingi sana umekuwa ukituambia USIOGOPE nasi twasema USIOGOPE imani yetu IPO kwako...
Comrade Lema... Umekuwa ukisema ni heri ya vita inayitafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu, ni maneno ya kijasiri yanayoweza kutamkwa na mtu mwenye hofu ya mungu kwakuwa anajua alitendalo...
Comrade Lema... Huna mfano wa kufananishwa kwasasa kwa aina ya siasa zako za level ya juu sana, pengine ni kwasababu unaongoza jimbo lenye Wananchi wenye uelewa mkubwa sana, ndiyo maana umekuwa ukifikiri makubwa wakati wote.
Comrade Lema... Wananchi wako wa Arusha mjini wanakupenda sana kuliko mtu mwingine yoyote yule mpaka imefikia mahali wanazuia wasije mahakamani siku ya kesi zako, Ila hakimu ameliona hilo na kukemea, huu ni upendo wa wazi kutoka kwa Wananchi wako Mpaka walikuweka ndani Wanaona wivu wanaamua kutumia nguvu kuwazuia...wanatamani wangependwa wao Ila haitawezekana kwakuwa Wanawaarusha wanakuamini wewe...
Comrade Lema: kwasasa kila Mwanasiasa kijana anatamani kufanya siasa kama zako, huu ni utukufu usiyolazimishwa bali umekuja wenyewe kwa upendo...
Comrade Lema... Uimara wako,ujasiri wako unazidi kutuimarisha na kutupa nguvu na sababu za msingi za kutokukata tamaa, Watu wanasema, kama Mbunge anaswekwa ndani kwanini Mimi Mwananchi wa kawaida niogope kwenda ndani kama sababu ya msingi ni kukataa uonevu au dhuluma...
Comrade Lema... Kukaa kwako ndani kumewatoa watu wengi hofu ya kutokukata tamaa ya kupigania mageuzi kwakuwa huko nako wanaishi binadamu wala siyo wanyama...
Comrade Lema.... Nakutakia ijumaa njema tutakutana jumanne Mahakamani nikiwa na makamanda wengi kutoka kila pembezoni ..... Ur Comrade Henry Kilewo
NEVER SAY NEVER
Godbless Lema ni Shujaa wa Siasa Tanzania Asiyepigia Goti Watawala
14
November 19, 2016
Tags
Kutukana watu ndio ushajaa Mheshimiwa ukizalilisha watu ni halali ukishughulikiwa ni haramu ujue kuandika habari zinavyolingana na tukio la mtuhumiwa
ReplyDeleteMshamba wewe na hao waliotukanwa
DeleteMjaze ujinga hivyo hivyo mwishoni ndio mtajua hasara zake.
ReplyDeleteGOOOOOODDDDD BLESSSS LDEMAAAAAAA!!!!!!!
ReplyDeleteHenery Kilewo,
ReplyDeleteUnajidanganya kufiri kwamba Tanzania ya sasa inaendeshwa kwa siasa uchwara kama hizi zako. Idadi kubwa ya watanzania wenye hekima na Roho ya Mungu na wala si kama hiyo yako/yenu ya Ibilisi wanatambua kwa yakini kwamba watu kama wewe na Lema ni watu msioitakia mema nchi na kustahili kushtakiwa na kufungwa kwa uchochezi ili wananchi waendelee kuijenga nchi yao wakiwa na amani.
Maana tumewachoka na tunataka muione ni ndoto kwa watu wa aina yenu kuiongoza nchi yetu.
We'mpe-sifa-za-kijinga huyo mjinga mwenzio asiyejitambua, ataendelea 'kunyea ndoo' kabla ya hukumu...eti comrade, comrade, comrade MAVI mfyuuuu.....MTU-MZIMA-HOVYO.......
ReplyDeleteHajatukana mtu
ReplyDeleteTatizo ccm na viongozi wake na vibaraka wao polisi na mahakimu uchwara wote
Anasenwa mungu sembuse vichwara hivi
Fyuuuuuuu
Nyie Jah people ni watu qa vioja. nilikuwa sijui kuwa lema pia ni Jah People. HASARA YENU.MIE SIMO
ReplyDeleteShujaaa ana nyea ndooo nyie mnakula bata ujinga mtupu
ReplyDeleteMandela alinyea ndoo naakaibuka shujaaa BABAUUUU!!!!! www baki kibaraka tu!!
DeleteAkili ni mali. Nasikitishwa sana na mambumbumbu wasio na kisomo, hekima akili wala ujasiri kwani ni janga kubwa la Taifa. Kwa miaka kumi Taifa limelea wajinga. Lema ni mfano wa hali ya Juu sana wakuigwa. Ester Bulaya pia ni Mwanamke shujaa sana si wale wanaolala bungeni na kupoka pesa tu. Wanaoangusha Taifa ni wale wanaopewa vyeo bila akili, uzalendo waoga na hawa ndio mizigo pia. Taifa litabadilika iwapo watu kama hawa na wengi Wapinzani wenye hekima.Watu watafika sehemu na kuelewa. Huwezi kumfungua macho kipofu na hata ukimgusa atakimbia akifikiri ni nyoka. ujinga huzaa ujinga.
ReplyDeleteHaya Mdau, Lema yuko katika lipi hapo. au ndiyo wale wale..Pole mwenzangu. we ni msomi au??? manake hata kilaza anajisema hivyo hivyo. kumbuka Tanzania yetu mpya itajengwa na mimi na wewe. HAPA KAZI TU
DeleteHuyu ni mtu wa Lupango. anapajua na anapapenda. hii yote ni kukimbia majukumu huku akitaka simanzi zetu. Tmekuchoka na vioja vya mheshimiwa. hapo ulipo ni pa saizi yako mpaka utakapo jirekebisha siasa si zako na huziwezi. pika mtori kwa mama ntilie tutakuja kukuungisha .haya ni maisha upo aise.Jiheshimu uheshimike filimbi nyingi mwisho goli linaingia Dimbani ukitahamaki solemba..MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE NA UDUMISHE AMANI YAKE.
ReplyDeleteAm sorry guys, sioni haja ya kupinga hisia za mtu mwache na hisia zake aweze kusemea na kusimamia sio kuanza kusodoa hisia zake. kama unataka awe vile unavyo amini kusingekuwa na maendeleo. mwaka 1901-1902 wanasayansi walikaa kujadili uwezekano wa kutengeneza ndege ya kupaa angani. walikuja na majibu kwamba haiwezekani lakini baadaye wanasayansi wawili (brown brothers) walianza majaribio yao mara baada ya hitimisho la wanasayansi. mwaka 1910 waliweza kupaisha ndege ya kwanza ambayo ili waacha wanasayansi midomo wazi.
ReplyDeletekwa hiyo dhana ya kudharau mawazo na mtazamo wa mtu ni jambo ambalo naona litafanya watu washindwe kuendelea. maendeleo yanaletwa na ukidhani wa kimtazamo na kimawazo. vinginevyo tutakuwa tunaishi maishi ya mkopo toka magharibi