Hali ya Mke wa Rais Magufuli Baada ya Kulazwa Hospitali ya Muhimbili

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo baada ya afya yake kuimarika.

Kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.

"Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara.

"Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth Magufuli.

Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi tarehe 09 Novemba, 2016 baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu akupe afya njema wewe ndiye nguzo yetu katika kumuona Baba anaendelea na uwajibikaji ipasavyo bila ya matatizo..mungi akulindeni wote..Amin

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad