Jay Dee Atiwa Hatiani, Atakiwa Amuombe Radhi Ruge wa Clouds FM

Mahakama ya Wilaya Kinondoni imemtia hatiani mwanamuziki nyota wa kike nchini Judith Wambura (Lady Jay Dee) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.Tokeo la picha la lady jaydee

Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi kupitia kwenye chombo cha habari chenye "coverage" pana nchini kote na ikiwezekana duniani.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.

Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jay Dee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa bado Wanaendelea Na season Yao tuu

    ReplyDelete
  2. du nimecheka mpaka basi eti ikiwezekana awaombe radhi duniani kote kwani duniani kote wanawafahamu hao? hao wanajulikana Clouds media Group tu sio kwengine, mimi mwenyewe siwajui hao ni kina nani halafu kwa sababu Jide ni mwanamke ndiyo mnataka aombe radhi ingekuwa mwanaume kamtukana mwanamke wala msingehangaika hata kuandika kwenye mitandao sababu mngeona ni sawa, kwani nyie wanaumme ndiyo kina nani? na sisi wanawake ni watu pia kama nyie, na hilo swala la kumpeleka mtu mahakamani sababu katukana ni Tanzania tuu ndiyo kuna upuuzi huo nchi za nje za wenzetu zilizoendelea hata ukimtukana polisi au mtu yeyote hupelekwi mahakamani kwa vitu vya kijinga namna hiyo ndiyo maana jela za kibongo watu wamejazana kibao sababu wengine wamewekwa pale eti sababu ya kumtukana mtu, Tanzania itaendelea lini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwahiyo unaona raha kwa wtu kutukanana hujui km matusi ni dhambi me mwenyew ni mwanamke ila kutukana si jambo jema ndugu yangu

      Delete
    2. HUJIJUI-KWAMBA-HUJITAMBUI......pole yako!

      Delete
    3. unayetetea matusi nawe inaonekana unapenda kutukana watu ole wako Ukonga inakungoja

      Delete
    4. nimewatukana watu wengi sana na pia nimemtukana mama yangu na mzee mwenye nyumba lakini sijapelekwa mahakamani hata siku moja

      Delete
    5. nimetukana watu wengi sana na sipelekwi Ukonga

      Delete
  3. Ulaya huwezi kupelekwa mahakani kwa kumtukana mtu, mambo hayo yanatokea bongo tu, nimetukana watu wengi sana na sijawahi kupelekwa mahakani, mtu akiniuzi huwa natukana

    ReplyDelete
    Replies
    1. tumekuachia umalize yote mtukanaji maarufu hongera pia kwa kutopelekwa maakamani il ipo ck yako

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad