Jela Mwaka Mmoja kwa Kumdhalilisha Mama yake Mzazi

Jela Mwaka Mmoja kwa Kumdhalilisha Mama Yake Mzazi
Mwanaume mkazi wa Ilala, Siwema Seif (40) amehukumiwa na Mahakama ya Mwanzo ya Ilala kwenda jela mwaka mmoja kwa kumtolea lugha ya matusi na kumdhalilisha kimwili, Zainab Ramadhan ambaye ni mama yake mzazi.

Akisoma hukumu mahakamani hapo jana, Hakimu wa Mahakama hiyo, Matrona Luanda alisema ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji, ulionesha kukosa shaka na kumtia hatiani mshitakiwa.

Shahidi huyo alisema siku ya tukio mshitakiwa alifika nyumbani kwao akaomba chakula akajibiwa kuwa kuna wali na mshitakiwa akasema hataki wali bali anataka ugali na mama akamjibu asingeweza kupika ugali na kumsisitiza Siwema ale wali.

Zainab alisema baada ya majibizano hayo, mshitakiwa alimtukana matusi ya nguoni mama yake, huku akisema hawezi kumzaa na kumkashifu kwamba hana sehemu ya kumzalia huku akitishia kumwua akiahidi kumtoa roho ndipo amjue yeye ni nani.

Kwa mujibu wa Zainab, alipoona ugomvi na matusi umezidi aliingia chumbani mwake, na ndipo mlalamikaji akamfuata na kumtukana huku akitishia kumwingilia kinyume cha maumbile.

“Baada ya hapo mshitakiwa alinivamia na kunidhalilisha kimaumbile kwa mikono yake,”alisema.

Baada ya ushahidi wa mama huyo dhidi ya Siwema, Mahakama ilitoa nafasi kwa kijana huyo kujitetea na Mahakama ikamtia hatiani.

Mwendesha mashitaka Blanka Shao alisema kwa kuwa japo mshitakiwa alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza, kitendo alichokifanya ni cha kifedhuli tena haonyeshi kujutia, alishauri apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake.

Hakimu Luanda alimhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kitendo alichomfanya mama yake mzazi.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 9 Ilala, mtaa wa Sophia Kawawa, nyumba namba 10.

My take:        kifungo cha mwaka mmoja hakitoshi

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haaaaa makubwa eeeehh shetani maluuni laaniwa kwa laana nzito ili usiwarubuni binaadam kwa ndimi zao. Huyu kifungo cha miaka 30 kwa vile alitaka kumbaka (rape) mwaka 1 atatoka akiwa na nguvu za sembe bovu la jela ili akammalize mamaake kwa kumuua.

    ReplyDelete
  2. kwakweli ni jambo lakuskitisha na la aibu, mwaka mmoja jela ni adhabu ndogo kwake kabisa

    ReplyDelete
  3. hayo yanatokana na malezi mabovu kutoka kwa wazazi, na si ajabu huyo huyo mama yake amemlea vibaya sababu kama huyo kijana angelelewa vizuri asingefanya ukatili huo wala asingeweza kumtukana au kujibizana na mama yake sababu ninao marafiki wengi wamelelewa vizuri na wazazi wao tangu wakiwa wadogo sijawahi hata siku moja kusikia kuwa marafiki zangu wana matatizo na wazazi wao tofauti na mimi, sababu mimi mama yangu alinisaliti nikiwa mdogo sana na aliniacha kwa ndugu kwa miaka mingi bila hata kujali nilikuwa na hali gani amekuja kunitafuta ukubwani na hata hajawahi kuniambia kwa nini alinisaliti nikiwa mdogo hata msamaha sijapata leo hii nimekuwa mtu mzima na maisha yangu halafu anataka kunipangia maisha yangu hicho kitu huwa kinaniuzi na ndicho kinanifanya niwe namtukana sana yaani sina heshima kwake na ndugu wananielewa siku moja alinifanyia matatizo nilimtukana sana mpaka nikamkatia mawasiliano sasa hivi hawezi kunipata katika simu na hakuna ndugu yeyote atakayempa namba yangu ya privat kwani mama ndiye kasababisha nisiwe na heshima kwa watu, wale walionilea waliona siyo majukumu yao kunifundisha mimi jinsi ya kuwaheshimu watu na ndiyo maana nina kiburi mpaka kumtukana ,nina bahati nina maisha mazuri na sijawahi kupata matatizo na watu, nina kazi nzuri na ninaishi mahali pazuri na maisha yanaendelea lakini kamwe sitaki tena mawasiliano na mama, na huyo kijana kwenye hiyo habari inaelekea ana hasira sana na mama yake hadi kufikia kufanya uamuzi huo na hivyo alivyofanya sio vizuri kama alikuwa na matatizo na mama yake ni heri angeenda kuishi maisha yake kukaa mbali na mama yake kuliko kufanya matatizo ambayo yamempeleka jela

    ReplyDelete
  4. ni aibu ila malezi yanachangia na laana ya familia unaweza ukakuta kwenye history ya familia yako kutoheshimu wazazi au wakubwa ni jambo la kawaida hivyo maombi ndiyo yatakayomkomboa Mungu ni jibu siyo jela kama tabia hata akitoka ataendelea tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad