Kamanda huyo amekiambia kipindi cha Sun Rise cha Times FM leo kuwa jeshi la polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida kilicho baki ni mwanasheria mkuu wa serikali kuandaa mashtaka kwa watuhumiwa.
“Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi kazi inafanyika, sasa huo ni wasiwasi kama wasiwasi basi unabaki kuwa wasiwasi, kikubwa niseme tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni. Yeye ni Mwenyekiti wangu wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana wasiwasi na chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya,” amesema Sirro.
“Lakini kama ana wasiwasi zaidi yeye ni kiongozi wetu atajua atachukua hatua gani dhidi yetu, kwa hiyo namuachia mkuu wangu wa kazi yeye ndio atajua nini cha kufanya.”
????????????????
ReplyDeletekamanda una busara sana!!
ReplyDeleteKam ni kweli waliokamatwa ni wengi na wako mikononi mwa vyombo vya usalama je ni kwanini wasifikishwe kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake?????? Ni kwa nini muruhusu hiyo hali ya kuumbuana mbele ya Waziri Mkuu juuu ya utendaji wenu wa kazi??????????? Mimi nadhani hapo kuna tatizo kubwa sana la kiuongozi na kiutawala; mawasiliano ni hafifu na utekelezaji wa shughuli zenu ni hafifu kabisaaaaaaa.......nadhani kuna mmoja wapo inabidi atumbuliwe kama sio Mkuu wa Mkoa basi awe huyo Kamanda Sirro. Na hiii itasaidia kuleta ufanisi wa shughuli za Kimkoa; Hayo malumbano ambayo yametokea mbele ya Waziri Mkuu ni dosari kubwa kwa utawala huu wa Awamu ya Tano.
ReplyDelete