KAULI ya Basata Kuhusu Video Mpya ya Wimbo wa Rich Mavoko na Diamond Platnumz

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambalo husimamia wasanii pamoja na kazi zao ikiwa ni wasanii wa filamu pamoja na wale wa muziki limesema kuwa linapitia video mpya ya mwanamuziki Rich Movoko aliyomshirikisha Diamond Platnumz kuona kama kuna vitendo vya udhalilishaji  wa kijinsia.

BASATA kupitia ukurasa wao wa Twitter wameandika kuwa wapo thabiti kusimamia maadili katika sanaa na udhalilishaji wa wanawake. Aidha wameeleza kuwa video hiyo iliyotoka jana usiku inayokwenda kwa jina la Kokoro ipo katika uhakiki kujionea kama picha za wanawake waliomo kwenye video hiyo zinakiuka maadili ya kitanzania na muda si mrefu watatoa taarifa.

BASATA wamekuwa wakiwafungia wasanii wengi wanaokiuka maadili ya sanaa ambapo miongoni mwa wasanii wengi waliofungiwa ni pamoja na Nay wa Mitego, Snura huku wengine wakipewa onyo na video nyingine kuzuiwa kuchezwa mchana kwa mfano Zigo Remix ya AY Ft. Diamond Platnumz na Asanteni Kwa Kuja ya Mwana FA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad