Kiwanda cha Saruji cha Dangote kimesitisha uzalishaji kutokana kuelemewa na gharama za uendeshaji hatua inayowaacha watumiaji wake njia panda.
Mwezi uliopita Kiwanda hicho kilililamikia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini(TPDC) kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara
Pia kiwanda hicho kinapinga uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo yapo chini ya kiwango na bei ghali.
Kwa nini serikali inapenda sana kuwa adui na wafanyabiashara! yaani wakishamuona mtu anafanya biashara wao kimbilio lao ni kuweka kila kitu bei juu! hawafikirii hawa watu wanaendesha vipi biashara zao ili tuwape unafuu wa wanachohitaji ili wao wapate faida na sisi tupate faida!! Ona sasa kinachotokea!!
ReplyDeleteHaya sasa gharama za uendeshaji......Kwani huyu mtu hakufanya upembuzi yakinifu (feasibility study) wa gahrama za uendeshaji kabla ya kuamua kuanzisha hicho kiwanda???????
ReplyDeleteHicho kisingizio cha kuuziwa gesi kwa bei nafuu hakiingiii akilini. Akumbuke biashara ya TPDC haitakiwi kupangwa na mtu yoyote yule na wala haipaswi kumpendelea Dangote eti kwa sababu ya Kiwanda chake cha Saruji. Akumbuke kuwa hilo Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania ni Shirika linalojiendesha kibiashara. Na pia kama ilivyo bishara nyingine linaangalia lifanye biashara kwa faida zaidi na sio kwa hasara.
Hadithi ya Makaa ya mawe pia haingiii akilini. Hasa katika kipindi kama hiki ambacho Serikali inaangalia katika kuwekeza katika viwanda na pia kuvilinda viwanda vya ndani ya nchi. Kwa hiyo sababu ya kuwa makaa ya mawe ni aghali na pia yako chini ya kiwango hicho ni kitu ambacho huyo Dangote alipaswa kukiona na kukifanyia kazi hata kabla ya kuanzisha hicho kiwanda chake hapo nchini. Hayo majumuisho yake yote alitakiwa awe ameyafanyia kazi kipindi kile cha feasibility study ambacho kingempa picha halisi ya uendeshaji wa hicho kiwanda hata kabla hajakianzisha.
Na kama Makaa ya Mawe ya Afrika ya Kusini ni ya bei rahisi na yana kiwango cha hali ya juu,kwa kulijua hilo ni kwa nini hakukianzisha hicho kiwanda chake pale Afrika Kusini?????????
Kisingizio cha kuwepo kwa viwanda vinavyotoa ajira kwa vijana wakati kimsingi na kiundani Taifa halinufaiki na uwepo wa hivyo viwanda hapa Nchi ni uongo na utapeli mkubwa na wa hali ya juu sana. Na pia ni hasara na hatari kwa ustawi wa Taifa la Tanzania.
Ni bora kusiwe na viwanda kabisa ili ijulikane kuliko kuwepo na kuvilea hivyo viwanda uchwara na vya kitapeli kama hicho cha Dangote.