Kocha Lwandamina Akanusha Kuja na Wachezaji wake Yanga

Klabu ya Yanga hii leo imemtambulisha kocha Geroge Lwandamina kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akirithi nafasi ya kocha wa zamani wa klabu hiyo Hans van der Pluijm ambaye amepewa majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya klabu hiyo.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema, anaamini Kocha Lwandamina atashirikiana na aliyekuwa kocha wa Klabu hiyo ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa benchi la ufundi Hans van der Pluijm ambaye anaielewa vizuri timu hiyo ili kuweza kuipeleka mbele zaidi.
Sanga amesema, wamefanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Klabu hiyo Hans na wameshabadili majukumu yake ndani ya klabu hiyo na Kocha Lwandamila amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Klabu.

Lwandamina amesema,anaamini Pluijm amefanya kazi nzuri na atahakikisha anashirikiana naye kwa kufuata nyayo zake na atashirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha Yanga inapata mafanikio zaidi.
Lwandamina pia amekana juu ya madai kwamba amependekeza wachezaji wawili aliokuwa nao Zesco United ya nchini Zambia kiungo Misheck Chaila na mshambuliaji Mkenya Jesse Were wasajiliwe pia ndani ya Klabu ya Yanga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad