Majambazi Yawachezesha ‘Kwaya’ na Kuwapigisha ‘Maombi’ Wenye Nyumba Kabla ya Kuwaibia

Baba wa familia iliyoporwa jana katika mtaa wa Epe mjini Lagos nchini Nigeria, amesimulia kuwa Majambazi waliwaamuru kushiriki nao kucheza kwaya na kumtukuza Mungu kwanza kwa maombi kabla ya kuwapora mali zao.

Bwana huyo aliyefahamika kwa majina ya Michael Oyuma, amesema majambazi hayo licha ya kuwa na silaha mbalimbali lakini pia kila mmoja alikuwa na biblia mkononi.

Amezitaja mali zilizoibiwa kuwa ni pamoja na simu za mkononi, Kompyuta mpakato mashine za mazoezi na za kufulia pamoja na fedha taslimu.

Taarifa inasema Majambazi hao waliendesha Ibada ya dakika 15 ‘Wakinena kwa Lugha’



Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii nayo kali nimecheka mpaka basi mijizi inatumia kila njia ya kuwaibia watu mimi naishi ulaya siku moja nilikuwa mjini wakatokea wanaijeria wawili wakajifanya wenyewe ni jehova wakataka namba yangu sikuwapa wakanipa namba yao wakasema eti niwapigie simu kuwa wanataka kuja nyumbani kwangu kuongea kuhusu neno la mungu mimi sikuwapigia simu nilijua tu kuwa wale ni wezi wanataka kuja nyumbani kuniibia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad