Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo baada ya kutuhumiwa kukusanya mapato kwa kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na Halmashauri inavyoagiza pamoja na kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu na kushirikina na wahalifu
Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kukaa muda mrefu bila kusoma mapato ya mtaa huo pamoja na kughushi stakabadhii za mapato.
Lawama hizo zimempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye yupo kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.
Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
HAPA KAZI TU. UNENEPE PEKE YAKO WENZAKO WAKONDEANA, WAPII
ReplyDeletehuu ndiyo uwajibikaji tunao utaka na mi message tosha kwa waliopewa dhamana za uongozi kuwa uwajibikaji na uaminifu na uadilifu na vigezo tosha kuendelea kuishikilia nafasi ya uongozi vinginevyo hatungoji habari ofisini tutazitafuta na kuzifata.. na usipo wajibika nafasi atapewa muaminifu na muadilifu next door. Ajira hazichezeqi wala kijinufaisha binafsi..Hongera MAKONDA NA UKO SAWA KIJANA. Hapa kazi tu. kila mmpja katika nafasi yake ya uwajibikaji
ReplyDelete