Mama Atukanwa Kwa Kumnyonyesha Mwanawe Mkahawani

Mama mmoja amezungumza baada ya kutukanwa kwa kumnyonyesha mwanawe ndani ya mkahawa mmoja huko Belfast.

Liz Skelcher alikuwa akimnyonyesha manawe wa wiki 11 Evie katika mkahawa wa Nandos wakati kisa hicho kilipotokea wiki iliopita.

Mkahawa huo umesema kuwa unaruhusu akina mama kunyonyesha wana wao

Lakini ilikuwa wateja wengine wa kike waliomtusi mwanamke huyo aliyekitaja kisa hicho kama cha kutisha na kushangaza.

Akizungumza na kpindi cha BBC cha Talkback, bi. Skelcher alisema: Nilikuwa katika mkahawa huo na mumewangu pamoja na mamake mume wangu wakati Evie alipoamka na akataka kunyonya,nilimuinua na kumuweka katika titi moja.

Mkahawa wa Nandos ambapo mama huyo alitukanwa kwa kumyonyesha mwanawe

Kulikuwa na wanawake watatu katika meza moja na mmoja wao hakupendelea mimi kumnyonyesha mwanangu.

Aliniambia kwamba tulikuwa tunamkera kumyonyesha mtoto katika mkahawa.

Aliendelea kunitusi mbele ya marafikize na alipoulizwa shida yake ilikuwa nini,alisema hakutaka kuona matiti yangu wakati alipokuwa akila chakula chake cha jioni.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ha ha ha ha pole yake labda hana mtoto huyo mama!!

    ReplyDelete
  2. huyo mama mtoto ni wake ila inafahamika kuwa wazungu hawapendi kumuona mtu akinyonyesha hadharani au mbele ya watu

    ReplyDelete
  3. mimi naishi Ulaya nina rafiki yangu ana mtoto siku moja tulipokuwa nje alimnyonyesha mtoto Wake huku akijificha alikuwa anaogopa watu watamuona na kumtukana, wazungu hawapendi kuona mtu akinyonyesha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad