Siasa za kutengeneza matukio ya kujiongezea umaarufu zinaanza kumwendea vibaya Lema.
Idadi ya watu waliojitokeza mahakamani katika kesi ya Lema leo imekuwa ndogo sana ukilinganisha na uhamasishaji uliofanyika.
Picha zinazorushwa kutoka maeneo ya mahakama hazioneshi zile "nyomi" tulizozizoea pindi Lema anapopelekwa mahakamani.
Hata wanachama kindakindaki wanaofuatilia kesi hii kwenye mitandao kama Facebook wamekuwa wakimtaja Bananga pekee kama chanzo cha taarifa kutoka mahakamani.
Hata tukio linalopewa umaarufu la mwanamke anayedaiwa kuzimia linaripotiwa kwa picha inayoonesha watu wachache sana wakiwa na mama huyo.
Muda umefika Lema atathmini siasa zake zisije zikampa maumivu makali kuliko matokeo yaliyotarajiwa.
By THINKINGBEING
Mbunge Godbless Lema Akipona Katika Hili Abadili Mbinu zake Katika Siasa
5
November 13, 2016
Tags
Huyu kwanza si Mtanzania kwani hata kauli zake si za kiuutu
ReplyDeleteMtu gani hata anasimama mbele ya wafuasi wake akitoa kauli za kutaka raisi afe au atakufa kisa ati madili yake ya umaarufu hayatimii
Lema na Lissu ni njaa inayoikabili siasa za upinzani BONGO
We pumbavu kweliiii lema ana kosa gani...kusema alichosema ndo kosa...au unatomboka upuuzi tu..umaarufu bado anao...haya kanye ukalale...
ReplyDeleteHuyu naye anajifanya eti na yeye kaishakuwa Nabiii kama T.B. Joshua. Hana lolote ni utapeli mtupu umemjaaa na tamaaa ya madaraka na pia ufisadi. Anajifanya kapewa maono na Mungu. Ni maono gani hayo ya kumtakia mtu mwingine kifo kama sio uchawi. Kama ni kweli ana maono kutoka kwa Mungu ni kwa nini asipewe maono ya kulitakia Taifa la Tanzania Amani pamoja na Maendeleo ya kweli kutoka katika lindi la umaskini linalowakabili Wananchi walio wengiiii????? Mbona hilo anashindwa kulizungumzia kama ni ono??? Yeye kwake ono ni kumtakia mtu mwingine Kifo tena hilo ono ni kwa Kiongozi wa Nchi anayepigania Maendeleo sawa kwa Wananchi wake na pia ni Kiongozi anayepigania maendeleo ya kweli kwa Taifa lake. Huyu mjamaaa kwa kweli ni mtu aliyechanganyikiwa na sana sana ni mchawi ambaye hatafika popote pale na maono yake feki. Sana sana atakufa yeye na kumwacha Mheshimiwa Magufuli palepale akijilia maisha yake.
ReplyDeleteHuyo toka zamani ni watu wenye wasiwasi na kuwa karibu na wahalifu na vikundi ambavyo ni hatarishi, kwa bahati mbaya hazikuchukuliwa hatua mapema dhidi yake. Kwa sasa inaanza kuonekana jinsi alivyo ila lazima aju kuwa kuna serikali na kuna historia ya watu ambao tena walikuwa na vichwa na elimu y hali ya juu lakini hawakufua dafu. Kwa bahati nzuri ameishajulikana na hakuna tatizo.Ila ajue maneno ya kusma kuwa rais atakufa ni maneno mazito kiusalama na hayawezi kuachwa hivihivi kwa sababu maalumu. Inatakiwa vyombo vya ulinzi na usalama vimhoji na aseme ni kwanini anasema hivyo na ikizingatiwa yeye ni kiongozi na anatazamwa na watu wengu nyuma yake, anazo sababu za kusema maneno hayo mabaya na siyo rahisi kumuachia kama hajasema ukweli, inaonekana sehemu hiyo inawza kuwa eneo hatarishi kwa nchi kama ilivyo MAIDUGURI nchini NIGERIA ambapo walijitokeza watu wa sampuli ya Lema na kuwa viongozi wa BOKO HARAMU ambao wanatishia usalama wa nchi hiyo, nao walianza kama LEMA, hivyo huyo hakuna kumlegezea afinywe hadi awe wazi hii ni serikali. Hya ni maoni yangu tu.
ReplyDeleteWell said
Delete