Wakati wa kulala si lazima wapenzi wafuate utaratibu ule ule kila mara.Hii inawezekana msimamo wa akili ulivyo kwa wakati huo.Fuatilia mitindo ya ulalaji na maana yake
KUKUMBATIANA
Mtindo huu hutumika sana kwa miaka 5 ya mwanzo wa ndoa.Mume huweka miguu juu ya mkewe na mikono kumkumbatia eneo la kifuani.Aina hii hupendwa sana na wanawake kwani hujiona yuko salama
Ni alama ya mahusiano bora ya kimapenzi.
KUTAZAMANA
Hukumbatiana lakini baada ya saa 2 au 3 hujibagua na kila mmoja kulala upande wake.Ni alama ya kusaidia kuondoa mkinzano unaoweza kujitokeza.
MALIWAZO YA MUME
Hushikana mikono na mke kuweka kichwa chake kwenye mabega au juu ya kifua cha mumewe.
Ni alama ya tafsiri ya mapenzi ya dhati ya mume kwa mke.
BARAFU WA MOYO
Mke hupanda juu ya mume na wanaweza kujadiliana mambo mbalimbali.Ni alama nzuri nyakati za maelewano.
KILA MMOJA UPANDE WAKE
Ikiwa mmoja kaweka mguu mmoja au mkono kwa mwenzake,mtindo huu hujulikana kama daraja la mahusiano.Si alama ya kutiliwa mashaka
USINGIZI BARIDI
Pale wanandoa wanapolala kama wasiotambuana bila kugusana pasipo kujielewa ni alama kuwa wako mbali kifikra.Hutokea pale mvuto usipokuwepo
Hali hii isiruhusiwe ikue.
VISIWA TOFAUTI
Wanalala bila ushirikiano kwa visingizio vya kuchoka,ni kama visiwa viwili tofauti.
Chanzo chaweza kuwa matatizo ya kimwili,kiakili au kiuchumi.Hali hii ikitokea mara kwa mara huweza hata kuachanisha wapenzi
MGONGO KWA MGONGO
Mtindo huu hujitokeza sana kwa wapenzi.Ingawa wanaweza kupeana migongo lakini wanaweza kuwasiliana.Ni alama ya kawaida na wanasaikolojia wanauita mtindo huu "muda wa kupumzika"
MZIGO USIOHITAJIKA
Kila mmoja hulala kivyake na mara nyingi ni kama vile wanandoa wanataka kuonyeshana umwamba.Kila mmoja hamjali mwenzake,,hali hii si ya kawaida ni mbaya sana kwani hutengana kuanzia wanapopanda kitandani hadi kunapokucha.Si ajabu hata kununua vitanda viwili au kulala vyumba tofauti.Wanasaikolojia wanaita hali hii kiburi na jeuri.