Mshindi wa Tuzo ya Nobel Wole Soyinka Adai 'Nitaondoka Marekani Trump akiapishwa'

Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka, anasema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais.

Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angeirarua green Card yake, ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika.

Soyinka alitoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza.

Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump.

Soyinka alishinda tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hilo.

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukitaka kuondoka USA ondoka kwani mwenye asara ninani. Trump ni msema kweli ndio maana watu wengi hawampendi, kwa mfanoTrump anahoji kwanini nchi nyingi za Afrika zilipata uhuru zaidi ya miaka 50 na mpaka sasa bado ni ombaomba!! Anasema kila mala akiangalia tv nchi za Afrika bado zinauwa watu mpaka watoto wasiokuwa na hatia, anahoji kwanini raia wengi wa kinaigeria ni matapeli na wezi wa kubwa!! Kwanini viongozi wengi wa Afrika wanag'ang'ania madarakani. Kama una mashaka na Trump una matatizo yako binafsi. Hapa kazi tuu

    ReplyDelete
  2. we nae fala tu anasema ukweli upi sasa anawabagua watu weusi hawapendi roho mbaya inamsumbua

    ReplyDelete
  3. Ukiwa na pesa unasema kila kitu

    ReplyDelete
  4. Mjinga mwingine na mwendawazimu,anambagua nani, Wajinga kama wewe hamko tayari kuambiwa kweli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad