MWAKA Mmoja wa Rais Magufuli Madarakani Umetosha Kumzika Lowassa Kisiasa

Sasa nimeamini hawa watu wako tofauti sana. Tena hawalingani hata kwa chembe. Watanzania hatukufanya Makosa kumchagua Rais Magufuli na kumkataa Lowasa. Katika huu mwaka mmoja wa utawala wa Rais Magufuli, hakika nimeona dhamira njema aliyonayo kwa Watanzania. Nimeona pia mantiki ya kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Katika Mwaka mmoja wa Rais Magufuli, mikakati imeshawekwa kwa ajili ya kujenga upya Reli ya Kati na Bomba la Mafuta kutoka Uganda. Miradi hii ikikamilika hakika Tanzania tutakuwa tunapata fedha nyingi za kigeni na hivyo kuweza kugharamia mahitaji mengi ya ndani.

Rais Magufuli pia kawaalika majirani zetu wa Rwanda, Zambia, Uganda, DRC na kaalikwa Kenya kwa lengo la kuhakikisha Wanafanya biashara na Tanzania na hivyo kutengeneza fedha lukuki.

Rais wetu pia kafanya mambo makubwa katika kubana matumizi yasiyo ya lazima. Nadiriki kusema kuwa Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli umetosha kumzika Lowasa kisiasa na sijui hata akigombea tena 2020 atakuja na sera zipi.

By Lizaboni/Jamii Forums

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hayo ni kweli na ndiyo habari yenyewe au tuseme kuwa HABARI NDIYO HIYO. HIYO NDIYO HABARI..MAGU NI HARI NYINGINE KABISA. EDO NI MWENZETU..NA ANAMKUBALI MAGU KWA KAULI YAKE. ALISEMA KATIKA SIFA ALIMPA MAGU KUWA CHARITY BEGINS AT HOME ALIPOFIKA CHATO..MAGU ANAKUMBUKA PIA..SIDHANI KAMA YEYE MWENYEWE HAMKUBALI MAGU..ILA WALIOMZUNGUKA KWA MATAKWA NA MALENGO YA KIBINAFSI..YEYE ANAJUA KUWA MAGU NI JEMBE LA MAJIRA YOTE HALINA KIANGAZI WALA MASIKA..HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  2. Kumzika vipi tena!! mbona bado anaishi na wanaokufa ni wale tu waliomtamkia vibaya kwenye uchaguzi..... au na wewe unataka kuwafuata?

    ReplyDelete
  3. Edo anakwenda kuchunga !!!

    ReplyDelete
  4. Muandishi anaongea mavii tena mavi yale ya asubuhi eti lowassa kasahaulika labda umemsahau wewe na mkeo...lowassa hasahauliki babu...neverr haitatokea labda afe..

    ReplyDelete
  5. Wewe Anoynymous ,November 30, 2016 at 2:43, unanivunja mbavu kwa kucheka ,maana jibu lako ni kama ulikuwa unamsubiri mtu azungumze kitu hicho,halafu unamtisha kuwa labda na yeye anataka kuwafuata?,nimecheka sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanaboa sana hawa jamaa na figisu figisu zao....

      Delete
  6. Aaahhh huyo naye. Mbona aliishakufa siku nyingi sana. Sana sana amebakia kama msukule fulani hivi......

    ReplyDelete
  7. Lazima ionekane hivyo, kwa sababu kakataza mikutano ya vyama vingine. Hebu acha aruhusu kila chama kiwe huru na shughuli zake bila kuingiliwa na polisi,ndio mpime.

    ReplyDelete
  8. √√√√√√√√√√√ Haki tena.

    ReplyDelete
  9. hivyo kweli mnaubavu wa kushiriki hoko 2025 ili hali mmejeruhiwa vibaya.. Muombe mungu nchi ilirudi salama na vyama vinavyo kosa vigezo vinafungiwa mkiwemo waleta fujo na mgawanyiko wa Amani yetu..Tathmini bado tunaendelea nayo!!!!!

    ReplyDelete
  10. hivyo kweli mnaubavu wa kushiriki hoko 2025 ili hali mmejeruhiwa vibaya.. Muombe mungu nchi ilirudi salama na vyama vinavyo kosa vigezo vinafungiwa mkiwemo waleta fujo na mgawanyiko wa Amani yetu..Tathmini bado tunaendelea nayo!!!!! Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad