Mwenyekiti Aomba Kupigwa Risasi Mbele ya Makonda Baada ya Kubanwa na Wananchi

Mwenyekiti soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani ameomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.
mokio-hassan
Mwenyekiti akijitetea mbele ya Wananchi

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.

Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa nafasi kwa wakazi wa Mbande hususan wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.

Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.

Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo ameuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona hajasema kuwa anataka kupigwa risasi au nyie udaku mmetunga wenyewe hiyo ya risasi?

    ReplyDelete
  2. Udaku mna mambo!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad