NDOA Yangu Imekuwa Chungu..Ndugu wa Mume Wamezidi, Nishauri Nifanyeje?

Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa, yaani ndio star kwao.

Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza.

Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe.

Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisa.

Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na ninaomba ushauri wenu ndugu ; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home.

Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.

Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.

Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!

Msaada jamani!

Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress

By Sisame

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na wewe zaa wengi uone hataleta mtu hapo na hiyo ndo dawa pekee

    ReplyDelete
  2. Kwa uchangiaji mzuri na ushauri ipeleke mada hii jamii forum, huko utapata washauri wa uhakika, jukwaa hili lipo zaidi kiudaku na kuwasifia au kuwakandia wasanii tu, vinginevyo tarajia kukatishwa tamaa tu

    ReplyDelete
  3. Njoo nikushauri physically

    ReplyDelete
  4. Yeuwiiiii pole dia pole mnooo article yako imenifanya nicheke na hapo hapo nahisi huruma kwako nacheka bkz napata picha mlivyo wengi na napata picha jins mumeo alivyo na wema wa ajabu kwa nduguze hata kwenye maandiko yamesema wema usizidi kipimo...sasa ushauri wangu ni huu...toka hapo haraka chukua mwanao nenda kwa msaada wa wazazi wako anza maisha mapy maana hakuna haja ya kuteseka hapo na ulishamwambia lakn haelekei yo too young to die wit stress...maisha yapo na ww ndo waku yaishi haya toka hapo nenda...na mwanao katulize akili ukifanya vibiashara vyako wakat mwingine tunaletewa majaribu kuonyeshwa hapo ulipo sipo sahihi...na unatakiwa kutoka kuendelea kukazana napo...nikujitafutia majanga mengine...i hope nimekusaidia

    ReplyDelete
  5. Kuwa muwazi kuwa kwa style hiyo ndoa itakushinda na umueleze mumeo kuwa mkiendelea kuendekeza ndugu hamtaendelea

    ReplyDelete
  6. JE MUMEO ANAKUPENDA KIDHATI?AU NDIO SABABU ZA KUTAKA MUACHANE?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad