PAUL Makonda "Mnasubiria Nitumbuliwe, Mimi Najua Nipo Kwa Kusudi la Mungu"

Baada ya kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha, Makonda afunguka.

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha Power BreakFast kinachorushwa na Clouds FM, Mkuu huyo amesema anajua kuwa kazi za serikali ni zakupita huku akidai yeye anamtegemea Mungu katika kazi zake.

“Mimi bahati mbaya ninajua kuwa hizi kazi ni zakupita watu wengine unakuta wanasema huyu jamaa atanyooshwa tu, atatumbuliwa, tutaona mimi sikomolewi kwasababu mimi najua nipo kwa kusudi la Mungu. Wakati wa Mungu ukipita mambo mengine yatajitokeza, lakini ninachokijua ni kitu kimoja asilimia 80 ya watu hawafanyi kazi ipasavyo katika ofisi zao,”

Aidha Makonda alisema ripoti nyingi anazoletewa zinaonyesha mtaani hali ni shwari lakini akienda kuzungumza na wananchi unakuta mambo tofauti na yale yalioandikwa kwenye ripoti.

Pia mkuu huyo amezindua kampeni iitwayo ‘Dar es salaam Mpya’ ambayo itamfanya kuzunguka katika sehemu mbalimbali za jiji hilo kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzipatia majibu.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lisemwalo lipo na kama halipo laja "time"ll tell"

    ReplyDelete
  2. Kama ni kweli ripoti unazoletewa mezani ni tofauti na hali halisi iliyopo mitaani ni kwa nini huwawajibishi hao watu wanaokuletea hizo ripoti????? Kwa nini usubiri kuwaaibisha kwenye vikao vya wazi tena mbele ya Waziri Mkuu??????........Na unafanya hivyo baada ya wewe kutishiwa kuwajibishwa?????? Au ndio zile za nani amfunge paka kengeleee???????

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani hapo nyie wote mnayo hayo majibu. Kuanzia Waziri Mkuu mpaka wewe Mkuu wa Mkoa na Kamanda wako wa Polisi. Ila ni kama mnatuzuga tu sisi Wananchi ama mnamzuga Magufuli. Inavyoelekea ni kama mlikuwa mnataka kufanya yenu ila ripoti zimemfikia Magufuli sasa mku hapo mnahanyahanya. Hamjui muanzie wapi kumrithisha bwana mkubwa kuwa nyie hamhusiki na huo ufisadi. Lakini kimsingi ripoti zimemfikia sasa tunabakia kuangalia huo mchezo utaaishia wapi. Kama ni kweli watu walikuja na nia mbaya ya kukuhonga je ni kwa nini hukuwawekea mtego wakamatwe?????? Kwa kweli chochote utakachokisema hakiingiiii akilini.

    ReplyDelete
  4. Tutaona mengi awamu hii
    Kuropoka ni awamu ya Tano
    Kama aliyewateuwa anasema hadharani kwamba viongozi aliowateuwa wakipendwa na wanainchi basi wana kasoro
    Hii inampa kichwa huyu bwana mdogo
    Anadharau hata awamu nne iliyomweka hapo alipo
    Angejuwa kassim ni nani angeufyata

    ReplyDelete
  5. Waziri alicho kisema ni wewe mkuu wa mkoa zuhia madawa ya kulevya, hakuna kiswahili kingine,kama huna uwezo ya kudhibti madawa ya kulevya achia wengine, hacha kumsingizia Mungu.

    ReplyDelete
  6. na utatumbuliwa tuu we ngoja ipo day utabugi step. kaz kuchongea wenzio uonekane msafii..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utasubiri sana bro, kama vipi we'saga chupa ubwie....... Makonda mbele-kwe-mbele

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad