Saida Karoli Adai Haujui Mkataba Aliosaini Meneja wake na Diamond Kuhusu Wimbo ‘Salome’ (Video)

Msanii wa zamani wa muziki wa asili Saida Karoli amedai yeye anasikia kama watu wengine kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond ameiangia mkataba na meneja wake wa zamani kuhusu kutumia vionjo vya nyimbo zake katika kutengeneza wimbo ‘Salome’ wa Diamond.
saida-karoli

Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’ ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye hilo.

“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”

Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.

Diamond na uongozi wake baada ya kuachia wimbo huo, walionyesha picha wakati wakifanya makubaliano na meneja wa zamani wa Saida.

“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,” Diamond alikiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahaaha make up ya dada nimeilewa lemba on fleek na viatu pia....ila huyu meneja wake looooh...alaaniwe..kama kachukua hela na hakumshirikisha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad