Samatta Acheza Dakika Sita Tu Genk Yaua 2-0 Ubelgiji

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda 2-0 dhidi ya AS Eupen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.

Samatta aliingia uwanjani dakika ya 84 kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis katika mchezo ambao mabao ya Genk yalifungwa na beki wa Mali, Ibrahim Diallo aliyejifunga dakika ya 20 na Alejandro Pozuelo dakika ya 38.

Huo unakuwa mchezo wa 33 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 13 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.

Katika mechi hizo, ni 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 15 alitokea benchi nane msimu uliopita na 12 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu.

Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Nastic, Colley, Brabec, Castagne, Ndidi, Pozuelo, Susic/Heynen dk65, Bailey, Buffalo dk76' Trossard) and Karelis (82 'Samatta).

KAS Eupen: Crombrugge, Diallo, Abdourrahman, Diagne, Lazare/Dufour), Garcia, Bassey, Sylla (80 Taulemesse) Onyekuru, Blondelle (88' Hackenberg) Oncansey.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad