SERIKALI Yapiga Marufuku Kusoma Degree Bila Kupita Form Six


Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katikals mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata degree za heshima zifutwe ni vigezo vipi kwa hao wanapata ?
    Wengi ni wanasiasa tu basi wawe na degree ya pili

    ReplyDelete
  2. Hii ni kurudisha maendeleo ya nchi nyuma.siku zote watu dunia nzima unaweza kwenda collage na kuunganisha mupata degree. Watu wenye akili na nia ya kujiendeleza wasikwamishwe na mtu mmoja. Hili siungi mkono inabidi lijadiliwe na si mtu mmoja aamue.Hili jambo ni zito na lismurupeshwe namna hii

    ReplyDelete
  3. safi sana lazima mwanafunzi azingatie mtihani wa Taifa
    manake ulikuwa unakuta mtoto ajibidiishi kufaulu mtihani wa mwisho akitegemea kuwa ataenda collage then afike degree
    na ukiangalia kwenye izo collage wanafunzi huwa hawafeli kabisa
    collage nyingi ni biashara za watu

    ReplyDelete
  4. HIYO IMEKAA VIZURI. KITU KIZURI TUUNGE MKONO. KWA NJIA HIYO HAKUNA KUBEBANA MAOFISINI BILA KUWA NA VIGEZO VINAVYOTAMBULIKA. MTOTO WA MASKINI KASOMA KWA SHIDA NA KUFAULU VIZURI LAKINI ANAKOSA NAFASI ILA YULE WA KUBEBWA KWA VISABABU FULANIFULANI KAFELI NA ANAWEKWA KWENYE NAFASI NZURI. HONGERAA KWA RAISI WETU MAGUFULI NA WAENDAJI WAKE WALIO MSTARI WA MBELE KUJENGA TANZANIA MPYA. KILA HERI NA MUNGU AWATANGULIE KATIKA KILA HATUA MNAYOPITA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad