Taarifa:Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Ujumbe Wake Hawakuzuiwa Kusafiri Uwanja wa Ndege Dar es Salaam

Jana Asubuhi iliandikwa Habari iliyokuwa imechapishwa kwenye gazeti la Tanzania la kila siku ‘Mtanzania’ ambapo kichwa cha habari cha taarifa hiyo kilikuwa kikisomeka ‘Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete azuiwa kusafiri nje ya nchi uwanja wa ndege Dar es Salaam.’

Katika habari hiyo, gazeti hilo liliandika kuwa kutokana na taarifa lililozipokea ni kuwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete na ujumbe waka jana walishindwa kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Abudhabi kupitia Dubai baada ya mmoja wa wajumbe aliokuwa ameambatana nao kutokuwa na viza ya kusafiria wakati wa ukaguzi.

Aidha, taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa hata baada ya mjumbe huyo kupata viza yake nusu saa kabla ya safari kuanza, walishindwa kuendelea kwani zoezi la ukaguzi wa abiria wanaosafiri na ndege hiyo lilikuwa limekwisha fungwa na ndege ikaondoka.

Kutokana na hali hiyo, gazeti hilo lilieleza kuwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete aliyekuwa ameambatana na mkewe pamoja na wajumbe wengine wangesafiri leo baada ya kukamilisha taratibu zote za safari.

Kwa taarifa za uhakika ambazo Swahili Times imethibitisha ni kwamba Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete na ujumbe wake hawakuzuiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na waliendelea na safari na ratiba yao kama kawaida bila ucheleweshwaji wowote.

Hii hapa chini ni picha ya Rais Mstaafu Dkt Kikwete akiwa katika banda la maonyesho la UNICEF Dubai leo asubuhi.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAMUMPENDI TU.WANOKO NYINYI/

    ReplyDelete
  2. Kwa miaka kumi kaiuza Tanzania, na muruhusu ufisadi ambso kutumbuliws ni kugumu sababu ya maingiliano kikazi na cheo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad