Tazama Video ya undani wa Msichana huyu Aliyebakwa Hadi Kufa – Makumira University

Mapema jana zimesambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).

Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi ya Leo akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo.

Hata hivyo Amenithibitishia kwamba Msichana huyo ni Mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila sio Mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai.

Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo.

Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.
 Sikiliza Hapa chini:
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. du bongo kwa unyama kumezidi na serikali iko wapi mpaka inafikia watu kuuliwa kinyama namna hiyo maana sasa hivi sio wezi ambao wanauliwa kikatili bali ni raia wema, serikali fanyieni kazi jambo hili serikali sasa ni wakati wa kuamka sababu hali hii ni tishio kwa wananchi Tanzania ya leo inatisha kwa ukatili kama huu mpaka watanzania waishio nchi za nje wanaogopa kurudi Tanzania kusalimia ndugu zao kwa ajili ya mambo haya ya kikatili

    ReplyDelete
  2. Masikini mtoto wa watu mi nahisi ni kama aliwatambua wauwaji wake ndio maana wakamuua. I hope waliohusika watakamatwa mara moja.

    ReplyDelete
  3. Vipi huyu mzungu mbona hajaulizwa. Kwa nini.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad