Baada ya kutolewa taarifa ya aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini, Moses Machali kuhusu kuunga mkono serikali ya awamu ya tano hivyo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi, Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ole Sendeka amezungumzia uamuzi huo.
Haya ndio machache aliyoyatoa Msemaji wa Chama cha Mapinduzi baada Machali kuhamia CCM akitokea chama cha ACT.
“Sisi kama chama cha mapinduzi tunaheshimu uamuzi wake na hatua ya pili kumpokea kwenye chama katiba za kikanuni zitafuatwa na hasa ukizingatia mimi namfahamu ni mtu mwenye msimamo, kwahiyo naheshimu maamuzi yake na hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa katiba na kanuni zetu za chama kuwapokea wananchama wanaoingia katika chama chetu kutoka upande wa vyama vingine,”amesema Sendeka.
Taarifa ya aliyekuwa mbunge wa Kasulu Mjini imetolewa na kiongozi huyo yeye mwenyewe.