UGONJWA Unaoambukiza Kama UKIMWI, Kati ya Watu 100, Nane Wanao

Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure kwa wagonjwa watakaobainaika kuwa nao kwa kutumia dawa ya Tenefovir katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia tarehe 1 December 2016.

Tanzania itakua nchi ya pili ukanda wa Afrika Mashariki kuanza kutoka huduma ya uchunguzi na matatibu ya ugonjwa wa Ini baada ya Rwanda ambayo imeshaanza udhibiti wa tiba ya ugonjw ahuo.

Kwa mujibu wa Dr. John Lwegasha ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Ini na Matumbo kutoka Hospitali ya Muhimbili amesema nchini Tanzania kati ya watu 100 watu nane wameambukizwa Virusi vya homa ya Ini.

Taarifa kamili ipo hapa. Bonyeza play kutazama
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani bongo iko mbali kwa kila kitu mpaka magonjwa ndiyo mnaamka leo kuwa kuna ugonjwa wa ini unaitwa hepatit huu ugonjwa umekuwepo kitambo kama ukimwi tu na si ajabu watu wengi tu bongo wamekufa na huu ugonjwa wa ini wa hepatit lakini ndugu zao wakafikiri kuwa wamekufa na ukimwi mimi mwenyewe ndugu yangu najua alikufa na huu ugonjwa huko bongo lakini ndugu wakaniambia kuwa ndugu yangu kuwa alikufa na ukimwi, hapa Ulaya tiba ipo ukionekana kama una huu ugonjwa wa ini unatibiwa unapona ikiwa si mnywaji sana wa pombe kama mtu unakunywa sana pombe inabidi uache kunywa pombe kwanza ndiyo upate matibabu, pia hapa Ulaya ukienda kupima HIV pia wanakupima na huo ugonjwa wa ini wa hepatit

    ReplyDelete
  2. Huu ugonjwa upo sanaa kusin mwa jagwa la Sahara African ndio kunaongoza asilimia kubwa ya mambukizi. Mambukizi yake ni ngono Pia na mengineyo kama kushea sindano . Haujulikani kivile kwenye jamii zetu ni kwa vile 90% up to 95% ya wanaopata mambukizi ya Ugonjwa huu asa wakubwa miili inapambana na virusi na kuwamaliza pasipo wenyewe kujijua kama walipata mambukizi ya virusi hao wa ugonjwa huu na kuwamaliza kabisa na kisha kujijengea kinga ya kudumu. Taabu inakuja kwa wale wenye kinga ndogo ya asili kutokana na magonjwa kama ukimwi na mengineyo na wathirika wengine kama watoto kutokana na kinga yao ni ndogo wako laisi kusumbuliwa na ugonjwa huu hadi kupelekea kupoteza maisha kwa nchi zilizoendelea. Wanatoa chanjo kwa umri wa vijana wadogo. Hauna dawa ya kuwamaliza virusi bali. Bali dawa za kuwatuliza virus wasiendelee kuzaliana na kuongezeka kulishambulia Ini zaidi. Kwani virusi hao wanapenda kuishi ndani ya Ini.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad