Unakumbuka Bifu ya TID na Dully Sykes...Dully Afunguka Haya

Hapo zamani, Dully Sykes na TID walikuwa kama paka na panya. Na sasa Dully ameibuka na kudai umri wake na pia kuwa na majukumu mengi, vilimfanya asione umuhimu wa kuendelea na tofauti zao.

Alikuwa akizungumza tofauti zilizopo kati ya Diamond na Alikiba na kudai kuwa ipo siku wakikua, wataacha.

“Hata mimi pia ilivyofikia kwenye age moja hivi nilikuwa na matatizo na TID, zamani. Lakini nilipoweza kukua niliacha hivyo, nilivyoanza kupata majukumu nikasahau kwamba tulikuwa na matatizo,” Dully alimweleza Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.



Ugomvi wa TID na Dully ulitokea mwaka 2002 wakati ambapo wote walikuwa wa moto na kushindanishwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee walipokuwa wakizindua album zao.

May 2014, Dully alikumbushia kuwa alimfunika TID kwenye show hiyo. Kauli hiyo haikumpendeza TID aliyeamua kujibu kwa kusema: TID unaweza kumfunika mzee Mnyama wewe? Alivaa nguo zake za Kariakoo, kama mapazia hivi,unafikiri Dully Sykes anaweza akanifunika mimi? Nimesoma shule za kishua, nimefanya muziki kwa intelligence, hao watu wa Kariakoo washamba.”

Naye Dully alijibu kauli hiyo ya TID kupitia XXL ya Clouds FM na kusema: Ngoja nikwambie kitu kimoja TID mimi nimempita miaka mingi, nimempita kila kitu yeye kanipita kasoma ndio alichonipita TID. Mimi kipindi hicho ndiye nimemkaribisha kwenye industry ‘mimi ndio Dully Sykes nipo juu mwaka 2002’, miaka mitatu nyuma mimi ndio nimetoka TID anatoka ndio nimemkaribisha. Halafu uzinduzi wetu TID alikuwa amelipa kosta mbili pale Magomeni akawaahidi atawapa hela wakifika pale Diamond round ya pili hajawapa hela ikabidi wale aliowaleta kwenye kosta mbili wamzomee yeye. Kwahiyo TID kaamua kuongea uongo. Halafu TID ni mdogo wangu anajua mimi ni kaka yake, historia ipo na picha ninazo. Mimi ndio nilipendeza kushinda TID. TID alikuja kama mgambo pale alikuja kama mgambo na nguo za mgambo nikisema mwanajeshi atakuwa juu kidogo. Mimi na miaka mitatu nyuma TID ndo anatoka 2002 na Zeze. Rafiki yangu kusoma hujui hata hata picha pia, inaeleweka na inajulikana kijana wangu mdogo ndio hivyo.”

Hivi karibuni bifu hiyo tena ilionekana kufufuka baada ya verse za Dully zilizokuwepo kwenye wimbo wa TID, Confidence alioshirikishwa Joh Makini kuondolewa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KAKA TID KILA MSANII KWAKO WEWE BIFU TU,MARA Q-CHILA LEO DULLY SYKES.MARA WEMA.KUWA KAKA TOA zeze jingine wachana kuwaste time.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad