VIDEO: “Mimi Sina Ugomvi na Profesa Lipumba” – Katibu Mkuu CUF

Kiongozi wa C.U.F Maalim Seif amekaa mbele ya Wanahabari November 27 2016 Dar es salaam na kuongelea mambo mbalimbali, miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni kama yeye na aliyekua Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Lipumba wana ugomvi?

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad amesema kuwa yeye hana ugomvi wowote na anayetajwa kwasa kuwa ndiye mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibahim Haruna Lipumba kama inavyodaiwa au kusemwa na wanachama walioko upande wake, isipokuwa tofauti ipo kati ya Lipumba, kundi lake na Chama.

“Mimi sina ugomvi na Lipumba hata kidogo, Lipumba ana ugomvi na chama na kundi lake maamuzi yamechukuliwa na mkutano mkuu wa taifa hata ukinikutanisha mimi na Lipumba siwezi kubatilisha maamuzi ya mkutano mkuu wa chama ambayo yaliwafukuza uanachama chini ya baraza kuu la uongozi” – Maalim Seif Hamad

VIDEO:

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee wangu bora ungeacha siasa kwa maoni yangu

    ReplyDelete
  2. Kama huna ugomvi na Lipumba mbona uliugomea mkono wa salamu kwenye mazishi ya mzee Jumbe?

    ReplyDelete
  3. Kama huna ugomvi na Lipumba mbona uliugomea mkono wa salamu kwenye mazishi ya mzee Jumbe?

    ReplyDelete
  4. Kama hujui usicomment, Seif hajagomea mkono wa Lipumba kwenye mazishi ya Jumbe, ila aliugomea mkono wa Shein

    ReplyDelete
  5. Kama hujui usicomment, Seif hajagomea mkono wa Lipumba kwenye mazishi ya Jumbe, ila aliugomea mkono wa Shein

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad