Walichoandika Diamond na Wema Sepetu kuhusu Ommy Dimpoz

Upo usemi kwamba fahari wawili hawakai zizi moja, ndicho kinaonekana kutokea kati ya mastaa wakubwa wa Bongo Flava nchini, Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz ambao waliwahi kuwa marafiki zamani, lakini sasa wamethibitisha wazi kuwa hawako poa kama mwanzo.

Kupitia Interview iliyofanywa ndani ya show ya XXL kupitia Clouds FM jana November 23, 2016, Diamond Platnumz alifungua kifua na kueleza mambo mengi sana juu ya tofauti yake yeye na Ommy Dimpoz ikiwemo lakini hakikuwekwa wazi sana chanzo cha kutofautiana kwao.

“Hivi jamani kweli mimi nigombane na Ommy Dimpoz kwasababu ya Wema Sepetu kweli? Siwezi kufanya hivyo. Mimi nafikiri tusilizungumzie nadhani wenye macho wameshanielewa kama hawajaelewa tangu jana waje kuelewa leo? watakuwa washaelewa. Dozen mimi naamua kumsitiri mwenzangu.” – Diamond

 Leo November 24, 2016 Ommy Dimpoz amepiga story na XXL ya Clouds FM pia, ambapo ameeleza kwa upande wake amepokeaje maelezo ya Diamond pamoja na ufafanuzi kuhusu ukaribu wake na watu ambao Diamond ameshatofautiana nao pamoja na kufanya kazi na Wema Sepetu.

“Mimi kwenda kushoot video ya Wanjera ndio ilikuwa sababu ya kutofautiana na Diamond, unajua mimi na Wema ni washkaji tangu hajaanza kuwa mpenzi wa Diamond, mimi nilimuweka Wema kwababu ana mashabiki wengi na nilitaka impact ya kazi yangu, mimi pia sijawahi kudate na Wema” – Ommy Dimpoz


Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KAMA SIO MWANAUME KWELI MPE ZARI ILI TUJUE KAMA SIO MZIMA ZARI ATATUTHIBITISHIA

    ReplyDelete
  2. Ukiwa star hutakiwi kumuabisha mwenzako ajabu sana hii!!!

    ReplyDelete
  3. Diamond is so big headed with his success. D ujue Mungu humpa mtu kitu kwa wakati wake. O hana dhambi ya kukuzidi na usihukumu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad