Wasira: Uzee Haunizuii Kudai Haki Yanu

Waziri wa muda mrefu na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira amewajibu wanaodai kwamba amelazimika kustaafu siasa baada ya mpinzani wake, Ester Bulaya kuwashinda wapigakura wanne waliokuwa wakipinga ushindi wake wa ubunge wa Bunda Mjini na kusema hajastaafu na uzee haumzuii mtu kudai haki yake.

Juzi, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilimpa ushindi Bulaya katika kesi ya uchaguzi hali iliyotafsiriwa na wadadisi wa kisiasa kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kisiasa wa Wasira.

Lakini jana, Wasira alipopigiwa simu na waandishi wetu kuelezea hatima yake ya kisiasa baada ya kesi hiyo, alisema wanaodai kuwa anatakiwa kustaafu siasa kwa sababu ni mzee hawana budi kuangalia kauli zao kwa sababu wapo wazee wengi anaowafahamu kwa majina na bado wapo madarakani.

“Suala la kusema nimestaafu siasa silijui na sijawahi kusema. Kesi hiyo inahusiana nini na siasa? Wapigakura wameona kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Hakuna uhusiano na uhusiano uliopo ni kwa sababu mimi ni shahidi na mimi niligombea,” alisema na kuongeza:

“Nataka wanipe ‘definition’ (maana) ya kustaafu siasa. Je, ni kunyamaza, nisitoe maoni. Mbona wapo watu walikuwa wanasiasa na bado wanatoa maoni ya kisiasa tena yenye manufaa makubwa?”

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Mzeee hivi hujaridhika tu na madaraka yote uliyowahi kuyapata. Wazeee wa Kitanzania mnataka mufe mkiwa bado na madaraka dah!! Hivi sisi Wananchi wa Kawaida ni kweli hatuhitaji kuwa na hayo madaraka na sisi tuingie kwenye hizo historia???? Kwa kweli tamaaa iliua fisi!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad