ALIYEBADILI Dini Afariki Baada ya Kubatizwa

Mkazi wa Mailisita wilayani Hai, Paulo (35) amekufa maji baada ya kuzama katika mto Kikafu, dakika chache baada ya kubadili dini na kubatizwa na maji ya mto huo kwa imani ya dini ya Kikristo.

Paulo ambaye jina lake la awali lilikuwa Issa Juma kabla hajabadili dini, alifariki Jumapili iliyopita katika mto huo, wakati shamrashamra za kubatizwa kwake zikiendelea pembeni ya mto.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lililazimika kuwakamata wachungaji wawili wa kanisa la Efatha waliombatiza lakini waliachiliwa baada ya Polisi kujiridhisha kuwa Paulo alikufa maji baada ya kubatizwa.

Habari zilizothibitishwa na Polisi, zimeeleza baada ya kubatizwa saa 8:30 mchana na wakati waumini wakiimba kwa ajili ya kurudi kanisani, ndipo Paulo na mwenzake waliamua kurudi kuogelea.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. INASIKITISHA SANA.

    ReplyDelete
  2. Wengine pia waende kubatizwa.pazuri hapo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HUYO ANAAMINI YUKO KWENYE UZIMA WA MILELE.NAWAPA pole ndugu na Jamaa wa Marehemu

      Delete
  3. Allah amuweke panapostahiki kuwekwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Allah ni mbora wa kulipa ujira, hakika atamlipa malipo yake. alicho panda ndicho atavuna

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad