Aliyetobolewa Macho Uso Kwa Uso na Scorpion Mahakamani


Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ imeendelea katika mahakama ya wilaya ya Ilala wakati shauri hilo lilipoletwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Wakati mshitakiwa akipandishwa kizimbani alidai ana wakili wake hivyo mahakama ilisubiri kwa muda wakili wa mshitakiwa Juma Nassoro na baada ya kufika mahakamani ndio kesi ilianza kusikilizwa.


Kesi hiyo ina mashahidi sita na mpaka sasa ameshasikilizwa mmoja ambaye ni shahidi namba moja Said Mrisho ‘aliyetobolewa macho’ ambaye leo December 14 2016 ametoa ushahidi wake mahakamani hapo akielezea tukio alilofanyiwa.


Baada ya kusikiliza kesi, mahakama hiyo imeahirisha shauri hilo hadi December 28 mwaka huu ambapo itaendelea na shahidi wa pili. 
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamani huyo anahitaji ushahidi wa nini imeshajulikana kamtoboa Said macho na kumletea ulemavu katika maisha yake yote sasa ushahidi wa nini tena mjue mnamuuza sana Said anaona kama mnamuonea pamoja na kuwa amepata ulemavu lakini bado tu li scorpion halijahukumiwa bado polisi huwa wanaangaika kuwatafuta majambazi sasa jambazi hilo hapo lakini mnashindwa kulifunga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad