AUNTY Ezekiel afunguka kuhusu mimba yake

Zile tetesi za muigizaji wa filamu nchini Aunty Ezekiel ni mjamzito huenda zikawa zimetimia baada ya kuficha kwa muda mrefu.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Aunty hajaweka wazi kama ni kweli ni mjamzito ila alichokisema ni kuwa anatamani tena kupata mtoto mwingine wa kike baada ya mtoto wao wa kwanza Cookie naye kuwa wa kike.

“I wish nipate mtoto wa kike tena, watoto wa kike hela ile, yaani mpaka wajae,” amesema muigizaji huyo.

Aunty Ezekiel ameongeza kuwa hataki kuweka wazi kama ni mjamzito kwa sasa ila watu watafahamu tu kwa kuwa hata mimba yake ya kwanza aliificha lakini watu waliweza kuibaini.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo ni kina rimbukeni hivo myi akiwa na mimba ni jambo kweli la kutangaza??? mimba haiji fich yanaka kujitangaza ovyo kuzaa ovyo kama paka bila ya ndoa hslafu wanajianika huo ni ushamba alafu eti wanajiita celebrities kutoka wapi? nendeni shuke mukasome kwanza munatia aibu tanzania celebrity anaulizwa neno very simple kwa kingereza hajui kujibu ana bakia mhh ooh yaa yaa yaa

    ReplyDelete
  2. Wote siyo wenye bahati ya kusoma na maisha siyo kusoma. Siyo kwamba wanataka kutangaza mimba ila nyie ndo mnazitafuta habari kwani mtu akiwa na mimba ni issue mpaka aanze kuhojiwa? Ustaaa mnawapa nyinyi mnaotafuta habari zao kaa kimya uone kama watakuwa mastaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad