BILA Tume Huru Wapinzani Wasahau Kuingia Ikulu – Kingunge

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika uchaguzi mkuu ujao.



Kauli ya mwanasiasa huyo mkongwe imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977, tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema Kingunge.

“Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana”.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee usituchanganye, kwani manake wateuliwa wa rais watakuwa wanaipendelea serikali? Na hiyo tume huru itakuwa inajilipa yenyewe?sio na serikali? Si itakuwa vilevile kama ndivyo unavyoona.

    Na ingekuwa kuna upendeleo kwa serikali basi wapinzani unaowasema wasingepata hata jimbo moja katika uchaguzi. Pumzika mzee!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upuuzi mtupu uliouandika hapo juu?
      Mzee yupo sahihi 100%...
      Angalia hapo kenya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anavyochaguliwa ndio uupate uelewa.

      Delete
  2. Mzee unataka kutuambia kuwa hukuwa mwadilifu katika kutenda kazi zako. Sera za ccm zinazotumika ziliasisiwa na nyinyi na Wewe mzee umechangia kuandika vitabu vingi vikiipamba ccm na kukisifia chama bora. Mliandaa misingi ya kukandamiza upinzani na kurithishana madaraka. Leo ktk umri huu unaona kuwa upinzani hauwezi kuingia ikulu bila kuwa na tume huru. Wapinzani walilalimika sana kuhusu tume huru toka kuanzishwa kwa viama vingi. Lkn mlikuwa bungeni kipindi chote na mlishirikiana sana kukandamiza upinzani kwa kura za ndiyoooo wengi Wape. Sioni Kama nia yenu ni njema kwa taifa.
    Katiba mpya nalo linanishangaza sijui uko upande wa rasimu ya waryoba au rasimu ya ccm Ambayo uliitetea na kupiga kura kana mganga wa kienyeji. Nakumbuka sana hotuba zako za kuipanga rasimu ya waryoba. Katiba pendekezwa bado imempa rais majukumu mengi tu. Sasa ww pia utuambie tupiganie katiba namna gani iwapo mchakato wa katiba mmeuharibu nyny kwa maksudi mkiwa ccm. ZambI za usaliti zitawatafuna Kama alivyosema baba wa taifa. Siasa za Africa kubadilka bila watu kumwaga damu ni ngumu. Kwa kweli mm Naona hata upinzani bado wakiachiwa nchi Hawawezi kutatua kero za mwananchi wa hali ya chini. Mifumo iliyoko si ya kitaifa bali ni ya kichama. Hivyo hakuna chama kisicho na mapungufu ya ubinafsi na kujiona kinafaa kuliko kingine. Kama taifa kwa nn tusitumie wasomi wetu kuanisha vipaumbele vya taifa kuliko kuwa na vipaumbele vya chama.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad