CALISAH Afunguka....Adai Wema Sepetu ni Msichana Mwelewa na Ana Mapenzi ya Kweli


Mwanamitindo aliyejipatia jina mwaka huu kutokana na kuwa na uhusiano wa muda mfupi na Wema Sepetu, Calisah, amemwelezea muigizaji na Miss Tanzania huyo wa zamani kuwa ni msichana mzuri na mwenye mapenzi ya kweli.

“Wema ni msichana mzuri, ana upendo, ni mwelewa, ana mapenzi ya kweli, sijaona kasoro kubwa ambayo yeye anayo kubwa tofauti na wasichana wengine,” amesema Calisah. “Ni msichana anayejua kucare, ana real love, pia ana mapungufu yake lakini mazuri ni mengi,” amesisitiza.

Model huyo ameongeza kuwa kwa sasa yeye na Wema hawazungumzi tena baada ya wiki kadhaa zilizopita kusambaa mtandaoni video inayowaonesha wakibusiana kwa mahaba mazito, kitu ambacho kilimkera Wema na kuvunja uhusiano wao.

Hata hivyo Calisah amekiri kuwa uhusiano wake na Wema umemuongezea umaarufu zaidi na kumrahisishia kazi zake.

VIDEO:MANGE KIMAMBI ACHOMA MOTO KADI YA CCM 

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. umemdhalilisha mtoto wa watu Wema, na haji kuongea na wewe tena na wala hujapata kazi yeyote tangu umdhalilishe mrembo Wema na hata sura ya uwanamitindo huna hata ngedere anayo sura nzuri kukuzidi wewe

    ReplyDelete
  2. eti umepata kazi tangu umdhaliliswe Wema kiss my ass hujapata kazi yeyote hamna mtu wa kukupa wewe kazi na Wema atahakikisha kuwa usipate kazi sehemu yeyote sababu Wema ni mwanamtindo wa muda mrefu anazo kontack na watu wengi, jinsi ulivyomdhalilisha katika social media Wema atahakikisha hautapata kazi yeyote mwishowe hautakuwa na sehemu ya kuishi utalala nje mshenzi mkubwa wewe, mwenzako Wema yuko anapiga kazi Nairobi anaingiza mkwanja mrefu lakini wewe umebakia kuongea na social media sababu hauna kazi ya kufanya,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad