CHADEMA yaijia Juu Serikali Kutoweka Kwa Kada Wake Saanane

Chadema kimeitaka Serikali kueleza kama imemkamata au inamshikilia kada wake Ben Saanane aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha mwezi mmoja uliopita.

Mbali ya kutaka Serikali ieleze mahali alipo msaidizi huyo wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, pia Chadema imetaka ufuatiliwe ujumbe wa vitisho aliowahi kutumiwa Saanane kupitia simu yake ya mkononi na mtu asiyejulikana.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema: “Serikali ina vyombo vya ulinzi na usalama, ituambie kama imemkamata au inamshikilia. Kama hawajamkamata watuambie mawasiliano yake ya mwisho yalikuwa lini na yalikuwa na nani na yalihusu nini.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad