Mbunge Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.
Rufaa hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.
Upande wa mtuhumiwa uliongezea muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda uliokuwa umepangwa awali.
Mbunge Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.
DHAMANI ya Mbunge Godbless Lema Yakwaa Kisiki Tena..Arudishwa Rumande
4
December 28, 2016
Tags
Duh kipindi hiki Lema kakiona cha mtemakuni
ReplyDeleteMBOWE HATA MAHAKAMANI HAONEKANI. JAMAA ANA ROHO MBAYA YULE. YEYE KAZI YAKE KUWAINGIZA WATU MKENGE TU
ReplyDeleteKwani Mbowe alimtuma atukane si kiherehere chake tu cha kutaka cheap popularity, wazee walituambia ulimi huponza kichwa.
DeleteKama huyu jamaa kasoma basi hakuelimika!!
ReplyDeleteMshamba sana jamaa huyu, he doesn't deserve his family!
I feel sorry for his poor wife and kids!
Wanateseka kisaikolojia ile mbaya yake!!