Dk Mwele Avunja Ukimya

Siku mbili baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Tiba na Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela, mwanasayansi huyo amesema yupo imara na atazungumza wakati muafaka ukifika.

“Kwa leo siwezi kuzungumza lolote kutokana na hali ilivyo, na namna jinsi watu wanavyoendelea kulizungumzia jambo hili lakini nitazungumza wakati ukifika na mtajua,” alisema

Dk Mwele kwa sauti ya uchangamfu.

Uteuzi wake ulitenguliwa Ijumaa usiku baada ya kutoa ripoti ya mwaka ya taasisi hiyo iliyoonyesha kuwa watu 80 waliofanyiwa utafiti waligundulika kuwa na virusi vya homa ya zika.

Taarifa ya utafiti huo ilionyesha kuwa kati ya watu 533 waliopimwa, 83 (asilimia15.6) walikuwa wameambukizwa virusi vya homa zika. Pia, kati ya watoto wachanga 80 waliozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali, asilimia 43.8 walikuwa wameambukizwa virusi vya homa ya zika.


VIDEO: Muigizaji Nisha bebee anywa mkojo wake kisa kumsahau mwanaume aliemuumiza moyo wake 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad