Rais mteule nchini Marekani Donald Trump amemteua Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Exxon Mobil, Rex Tillerson kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Tillerson(64) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi ya Texas, Marekani . Pia, miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa duniani.
Tillerson anatajwa kuwa na uhusiano mwema na rais wa Urusi Vladimir Putin jambo ambalo limewatia wasiwasi wa wana Democrat na baadhi ya wa Republican
Uteuzi huo unahitaji kuthibitishwa na bunge la Senate.
Siku chache zilizopita ilibainika kuwa majasusi nchini Marekani wanaamini kuwa Urusi ilihusika na kushawishi ushindi wa Trump.
DONALD Trump Amteua Tajiri Kuwa Waziri wa Mambo ya nje Marekani
0
December 14, 2016
Tags