Dr MWELE Malechela(Aliyetumbuliwa) : Safari Itasonga Kwa Msaada wa Mungu

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr Mwele Malechela, ametoa kauli yake baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Dkt John Magufuli, Ijumaa hii.

Kutenguliwa kwake kumekuja siku moja tu baada ya kuzungumza na waandishi na kudai kuwepo kwa virusi vya Zika nchini. Alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi hivyo. Taarifa yake, ilikuja kukanushwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Akijibu tweet iliyosema, ” Pole sana @mwelentuli safari yako na isonge mbele Dada,” Dr Mwele amesema, “Ahsante na itasonga kwa msaada wa Mungu.”

Tweet nyingine alijibu: Ahsante Mathew. Nilipewa dhamana nimetumikia ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kutumikia WaTanzania kupitia utafiti.”
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na mtakufa sana mwaka huu mnabishana na watafiti ambao ni wataalamu.

    ReplyDelete
  2. Muwe mna hakiki habari kabla hamjazitoa. Hiyo picha ina uhusiano gani na hii habari????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndo uandishi wa kitanzania huu hakuna taaluma

      Delete
  3. Wafanyakazi wa serikali kuweni makini na hiki kijamaa hakitaki mchezo na kazi

    ReplyDelete
  4. Taaluma ya kweli huwa haidanganyi. Taaluma siyo siasa. Tukae na tusubiri. Wanataaluma wameshasema.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad